Rapcha Amjibu Dizasta Vina Kwenye Nyu'clear Freestyle

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ushindani unaendelea kupamba moto kati ya Rapcha wa Bongo Records pamoja Dizasta Vina na hii ni baada ya hivi karibuni Rapcha kuachia ngoma mpya ambayo ndani yake amemjibu Dizasta Vina.

Siku chache zilizopita rapa Dizasta Vina alitoa Best Friend, ngoma ya Dakika 8 ambayo ilikuwa na lengo la kumjibu Rapcha, kwani kabla ya hapo Rapcha aliachia ngoma ya kuitwa Story Nyingine Freestyle ambayo ndani yake alimkosoa Dizasta Vina.

Ukinzani kati ya Dizasta Vina na Rapcha ulianza baada ya Rapcha kuachia "Story Nyingine" na katika moja ya mstari wa ngoma hiyo, Rapcha alionesha kuchukizwa na kitendo cha Dizasta Vina ku-like kupitia Twitter, ujumbe ambao ulikuwa unamshusha yeye thamani ambapo Dizasta Vina alijibu suala hilo kwenye Best Friend na siku ya leo Rapcha ameachia hii "Nyu'clear" Freestyle kuendelea mpambano.

Ndani ya Nyu'clear Rapcha amezungumzia kuhusu uwezo wake mkubwa alionao kwenye Hip Hop ya Tanzania huku akiwa anatoa ushauri unaoudhi kwa wapinzani wake kwenye muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=-LVn3zhJAR0

Leave your comment