Rapa Billnass Aweka Rekodi Mpya Youtube Mwezi Desemba

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki na rapa kutokea Tanzania, Billnass ameendelea kuimarisha nafasi yake kwenye muziki wa Bongo baada ya kuweka na kutengeneza rekodi mpya kwenye mtandao wa Youtube kwa nchini Tanzania.

Hivi karibuni Billnass ameachia ngoma yake ya  Puuh ambayo amemshirikisha Billnass na tangu kuachiwa kwake, Puuh imekuwa ni ngoma pendwa sio tu kwa wanaume lakini pia kwa mabinti wengi ambapo kupitia mitandao kama Snapchat, Tiktok na Instagram, ngoma hiyo imefanya vizuri.

Kwa mwezi Desemba 2022 Billnass ameongoza kwenye orodha ya wasanii wa Hip Hop Tanzania waliotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube ambapo kwa mwezi huo pekee amekusanya watazamaji takribani  Milioni 2.4 hivyo kusimamia kama msanii wa Hiphop aliyetazamwa zaidi Youtube kwa mwezi Desemba 2022.

Katika orodha hiyo ambayo Imetolewa na Chart Data, Kontawa alishika nafasi ya pili akiwa na watazamaji Milioni 1.36 akifuatiwa na Mwana FA, Darassa, Professor Jay na Msodoki Young Killer.

Aidha kwa mwaka 2022 Puuh ya Billnass  ndio ngoma ya Hip Hop iliyowahi kufikisha watazamaji Milioni 1 kwa haraka zaidi Youtube baada ya kufanya hivyo ndani ya siku 12 tu.

https://www.youtube.com/watch?v=3qN9A3XIPcw

 

Leave your comment