Mavokali Amshirikisha Rayvanny Kwa Wimbo ‘Mapopo’ , 'Commando' Remix

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Fundi wa muziki kutoka Tanzania Mavokali kwa mara nyingine ameingia kwenye vichwa vya habari nchini Tanzania baada ya kuachia  Commando Remix ambayo amemshirikisha Rayvanny na kuipa jina ‘Mapopo’.

Ngoma ya Commando ya Mavokali imepata mafanikio makubwa tangu kuachiwa kwake ikiwemo mastaa wakubwa duniani kama DJ Khaleed walionekana wakitumia ngoma hiyo kucheza katika mitandao ya kijamii. Aidha ngoma hiyo ya Commando ilionekana kusikilizwa zaidi kwenye mtandao wa Shazam ambapo ilionekana kutamba huko Saudi Arabia, Columbia, Peru, Venezuela na nchi nyingine nyingi.

Hii leo Mavokali na Rayvanny wameshirikiana ka maudhui ya msimu wa Krismasi. Video hiyo imesheheni uzuri wa kimavazi na hata mistari ya mapenzi. Kama kawaida Rayvanny ameonyesha ustadi wake katika katika wimbo hii.

Kwa mara nyingine tena Rayvnny atakuwa ameshirikishwa kwenye ngoma nyingine na wasanii wa Tanzania tangu kuigura WCB. Mwaka huu kwani mpaka sasa ameshashirikishwa na Billnass kwenye Utaonaje, Mabantu kwenye Star Remix pamoja na Pheelz kwenye Finesse Remix.

https://www.youtube.com/watch?v=v0bBHiz3Pds

Leave your comment