Dully Sykes Adokeza Collabo Na Diamond Platnumz

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Dully Sykes hivi karibuni amedokeza kwamba kuna collabo kubwa inakuja kati yake na CEO wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz

Dully Sykes ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya "Do Do" akiwa amemshirikisha Kusah amezungumza hivi karibuni kuhusu ngoma yake na Diamond Platnumz na kudokeza kuwa ngoma hiyo imechelewa kutokana na ratiba za Diamond Platnumz.

"Sina wasiwasi na wimbo wetu, wimbo wetu ni mzuri na namsubiri Diamond kwa sababu siwezi kum-rush kwa sababu ana mambo mengi ni mtu wa kusafiri sana, mtu mwenye mipango mingi kwa hiyo ni subira" alidokeza Dully Sykes ambaye alianza muziki rasmi mwaka 1997 kuelekea 1998 na alipata umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Dully Sykes pia aliwatoa hofu mashabiki zake kwa kusema kuwa kutokana na ukubwa wa Diamond Platnumz, collabo hiyo hata ikiachiwa mwaka 2024, bado itafanya vizuri.

"Tukiwazungumzia wasanii Tanzania International Diamond nae ni International. Msanii kama Diamond wimbo wake hata nikiutoa 2024 ambao nimefanya nao utakuwa kuwa hit tu." alizungumza Dully Sykes.

Kando na Dully Sykes, wasanii wengine kutoka Tanzania ambao tayari wana ngoma na Diamond Platnumz lakini bado haijatoka ni pamoja na Marioo pamoja na G Nako.

Leave your comment