Aslay Aachia Ngoma Mpya Follow Me Akiwa Na Harmonize.

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye mwanamuziki kutoka Tanzania, Aslay, kwa mara nyingine ameweka historia mpya kwenye Bongo Fleva baada ya kuachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Follow Me ambayo amemshirikisha CEO wa Konde Gang, Harmonize.

Follow Me ni ngoma ambayo Aslay anatumia vionjo vya Bongo Fleva ili kufikisha ujumbe ambapo ndani ya wimbo huu, Aslay pamoja na Harmonize ambaye anasikika zaidi kwenye verse ya pili wanaapa kutoa mapenzi kemkem kwa wenza wao huku wakiwaomba "wawafuate" ili watengeneze maisha.

Mashahiri mazuri, muingiliano mzuri wa sauti kati ya Harmonize na Aslay pamoja na ujumbe unaopatikana kwenye "Follow Me" bila shaka vimechagiza ngoma hii kuwa bora sana.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Aslay kuachia ngoma ilikuwa ni mwaka 2021 alipoachia Nashangaa, ngoma ambayo ilipokelewa kwa ukubwa sana, na mashabiki wa muziki wa ndani na nje ya Tanzania.

Aslay ni moja kati ya wasanii wakubwa nchini Tanzania ambaye alipata umaarufu tangu akiwa na umri mdogo na kisha baadae kujiunga na Ya Moto Band, kundi la muziki ambalo baada ya kufanya vizuri kwa takriban miaka 4 lilibunjika na kupelekea Aslay kuanza tena kufanya kazi peke yake.

Tangu kundi la Ya Moto kuvunjika, Aslay ametoa ngoma mbalimbali kama Likizo, Mchepuko, Naenioy, Hauna na ngoma nyingine nyingi ambazo zilichagiza yeye kuwa msanii pendwa baina ya mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=E56hS8WcVGc

Leave your comment