Rose Muhando Aachia Tracklist Albamu 'Secret Agenda'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli wa Injili kutoka Tanzania Rose Muhando hivi karibuni ametangaza orodha ya nyimbo ambazo zitakuwepo kwenye albamu yake ya Secret Agenda ambayo inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Rose Muhando ambaye mara ya mwisho kuachia kazi ilikuwa ni miezi miwili iliyopita pale alipoachia wimbo wake wa Funguka ametoa taarifa hiyo ikiwa ni siku tatu tangu atangaze kwamba albamu yake ipo tayari na itatoka kabla ya mwaka huu 2022 kuisha.

Akizungumzia kuhusu albamu hiyo ambayo ameipa jina la Secret Agenda, Rose Muhando kupitia akaunti yake ya Instagram alidokeza kwamba albamu hiyo itakuwa na ngoma 12 ikiwemo Siki Na Sifongo, Ombi Langu, Secret Agenda na nyinginezo nyingi huku nyimbo zote akiwa ameimba mwenyewe bila kufanya collabo.

Kando na albamu hii, Rose Muhando pia kufikia sasa ameshaachia albamu tofauti tofauti kama Uwe Macho (2006), Jipange Sawasawa ya mwaka 2009 ambayo ilisheheni ngoma mbalimbali kama Nibebe, Mungu Wa Mapendo na nyimbo nyingi.

Aidha msanii mwingine ambaye anatarajiwa kuachia albamu hivi karibuni ni Christina Shusho ambaye mapema mwezi huu alitangaza kwamba albamu yake ya Hararat itaachiwa hivi karibuni.

Leave your comment