Hatimaye Rosa Ree Aachia Albamu Yake Ya "Goddess"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mambo yameendelea kuwa sukari kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania na hii ni baada ya rapa nguli kutokea nchini humo, Rosa Ree kuachia albamu yake ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu ya kuitwa "Goddess".

Rosa Ree ambaye miezi michache iliyopita alitajwa kuwania tuzo za AFRIMMA kama rapa bora Afrika ameachia albamu hiyo ya Goddess ikiwa ni albamu yake ya kwanza tangu aanze safari yake ya muziki. Rosa ree alidokeza kuhusu ujio wa albamu hii tangu mwaka 2021 kupitia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari.

Albamu ya Goddess imesheheni ngoma 17 za moto huku akiwa ameshirikisha wasanii tofauti tofauti kama Ibrah Jacko, Christian Bella, APass, Fid Q, Fik Fameica, Ssaru, Spice Diana pamoja na Cherry huku collabo yake na Fid Q ikiwa ni moja kati ya ngoma ambazo zimekuwa zikisubiriwa sana kwenye albamu hiyo ambayo uzinduzi wake ilifanyika Terrace Lounge.

Aidha Goddess imetayarishwa na mafundi tofauti tofauti wa muziki kama Pancho Latino, Ibrah Jacko, Paul Maker, Breezy International pamoja na Joga Beats. Kwa albamu hii Rosa ree anaweka historia ya kuwa katika ya wasanii wachache wa kike wa Hip Hop kutoka Tanzania kuachia albamu ya muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=x58k-CHH_Ps

Leave your comment

Top stories

More News