Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia 'Shetani' Video

[Picha: Screengrab/Youtube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kunako lebo ya WCB Wasafi Mbosso Khan hatimaye ameachia video ya ngoma yake ambayo inasumbua Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ya kuitwa "Shetani"

Mbosso ambaye kabla ya kuingia kwenye lebo ya WCB Wasafi alikuwa anahudumu kwenye kundi la Ya Moto Band ameachia video hii ya Shetani ikiwa ni video yake ya kwanza kutoka kwenye Khan EP pamoja na Video yake muziki ya pili kwa mwaka huu baada ya Moyo ambayo kufikia sasa imejizolea mamilioni ya watazamaji huko Youtube.

Kama ambavyo mdundo wake ulivyo, video ya Shetani inamuonesha Mbosso akiwa anacheza na "madancer" wake wa kike kwa wa kiume katika maeneo mbalimbali huku Costa Titch akikoleza hadithi nzima ya video hiyo kwani anaonekana akiwa anaimba na kufurahi kwenye saluni ya kiume.

Ukiweka kando mitindo mzuri ya kucheza, inayopatikana kwenye video hii, upangiliaji wa matukio, hadithi nzuri pamoja na ubora wa picha umechagizwa kazi hii mpya ya Mbosso kuwa ya kipekee sana.

Video ya Shetani ya kwake Mbosso imefanyika huko Afrika Kusini na imeongozwa na Lotus Sutra ambaye kando na video hii poa ameongoza video nyingine nyingi ikiwemo Super Star ya kwake Costa Titch akiwa na Diamond Platnumz, Just Do It ya Costa Titch na video nyingine nyingi.

https://www.youtube.com/watch?v=KhNzgS38c3Y

Leave your comment