Aslay Afunguka Chanzo Cha Yamoto Band Kuvunjika
23 November 2022
[Picha: Screengrab/Youtube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Mwanamuziki kutokea lebo ya Rockstar Africa na ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa kimya, Aslay kwa mara ya kwanza ameweka wazi sababu hasa zilizochagiza Ya Moto Band kuvunjika na kuamua kuanza kufanya muziki peke yake.
Kundi La Ya Moto liliundwa na wasanii wanne ambao ni Aslay ambaye alikuwa ni kiongozi, Beka Flavour, Enock Bella na Mbosso ambaye kwa sasa yuko WCB Wasafi lilipata, umaarufu mkubwa mwaka 2013 baada ya kutoa wimbo wa "Ya Moto" na tangu hapo walitikisa Tanzania na ngoma zao mbalimbali kama Nitakupwelepweta, Nisambazie Raha, Niseme na nyinginezo nyingi.
Katika Makala yake ya hivi karibuni, Aslay amedokeza kuwa kilichofanya Ya Moto Band kuvunjika ni baada ya kundi hilo kuwa kubwa na kila mtu kutaka kutamani kufanya kazi peke yake na hiyo ni baada ya mashabiki kuanza kuwasifia kila mmoja kivyake na kuanza kuwashindanisha.
"Kila mtu tena mafanikio yalivyokuwa makubwa alikuwa anatamani kujiona yeye kama yeye sasa amefika sehemu gani. Kila shabiki anamsifia mmoja wa Ya Moto Band kwa wakati wake kwa hiyo wakawa wa najiona tayari nishakuwa mkubwa na kuna baadhi ya mambo mengine yalitokea mawili matatu nahisi yalisababisha kundi letu kuvunjika tayari" alizungumza mwanamuziki huyo.
Tangu kuondoka Ya Moto Band mwishoni mwa mwaka 2016, Aslay ametoa ngoma kali mbalimbali ikiwemo "Kwa Raha", "Nyang'anyang'a" na ngoma nyingine nyingi ambazo zilitikisa Afrika Mashariki.
Leave your comment