Hawa Ndio Watanzania Walioshinda Tuzo Za Afrimma
23 November 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Tuzo za AFRIMMA zilirindima wikiendi hii siku ya Jumamosi huko nchini Dallas Texas nchini Marekani ambapo wasanii wengi kutokea Tanzania wameweza kushinda tuzo katika tuzo hizo ambazo zina lengo la kuwaheshimisha na kutambua mchango wa wasanii mbalimbali Tanzania.
Kwa nchini Tanzania watu mbalimbali maarufu walishindwa tuzo kwa mwaka ikiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Diamond Platnumz, Rayvanny pamoja na Zuchu ambaye pia kwa sasa anaendelea na ziara yake ya kimuziki huko nchini Marekani.
Zuchu alishinda kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki, kipengele ambacho alikuwa anachana na wasanii kama Jovial na Femi One kutokea pamoja na Maua Sama na Nandy kutokea na hii ni mara ya pili kwa Zuchu kushinda tuzo hizo kwani mwaka 2020 alishinda kama msanii bora chipukizi.
CEO wa Next Level Music Rayvanny aliibuka kama msanii bora wa kiume Afrika Mashariki akiwashinda wasanii wengine kama bosi wake wa zamani Diamond Platnumz. Aidha katika hafla ya tuzo hizo, Rayvanny alitumbuiza wimbo wake wa Mama Tetema bao amemshirikisha Maluma.
Rais wa Tanzania, Mheshimiwa, Samia Suluhu Hassan alishinda tuzo ya kiongozi bora Afrika kutokana na mchango wake uliotukuka kwenye sekta ya muziki Tanzania. Tangu kuingia kwake madarakani Rais Samia amechukua hatua stahiki kuhakikisha sekta ya kimuziki inakua. Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kurudisha tuzo za muziki nchini maarufu kama Tanzania Music Awards ambazo zilisimama mwaka 2015.
Diamond Platnumz ameibuka kidedea kipengele cha mtumbuizaji bora Afrika, kipengele ambacho pia alishawahi kushinda mwaka 2015 kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards maarufu kama MAMA.
Leave your comment