Rosa Ree Kuachia “Goddess” Album Wikendi Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya subira muda mrefu, rapa kutokea Tanzania Rosa ree hatimaye amepoza shauku ya mashabiki zake baada ya kutangaza kwamba albamu yake ya kuitwa Goddess itatoka hivi karibuni.

Rosa ree ambaye pia amechaguliwa kuwania tuzo za AFRIMMA kama rapa bora wa kike Afrika, kupitia Instagram akaunti yake ametangaza kwamba albamu yake itaitwa Goddess na pia ameweka wazi wasanii walioshirikishwa kwenye kazi yake hiyo mpya.

Albamu hiyo ya Rosa Ree imesheheni ngoma 17 na ndani yake wasanii tofauti tofauti wameshirikishwa ikiwemo Ibrah Jacko, Appy, Christian Bella, A Pass, Fid Q, Nadia Mukami, Fik Fameica, Spice Diana na wasanii wengine wengi.

Akizungumzia kuhusu albamu hiyo, Rosa Ree alitanabaisha kwamba imechukua takriban miaka minne kuandaa albamu na kwamba kwenye albamu hiyo mashabiki zake watapata kuona kusikia hadithi mbalimbali za Rosa Ree akiwa kama Mama, Msanii na maisha yake kwa ujumla.

Ikumbukwe kwamba wasanii kutoka Tanzania ambao wanatarajiwa kutoa albamu hivi karibuni ni pamoja na Marioo na albamu yake ya The Boy You Know pamoja na Jux ambaye ndani ya wiki hii atadondosha albamu yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya kuitwa "King Of Hearts".

Leave your comment