Nyimbo Mpya: Jux 'Wena','Baby Boo' Mr. Blue na Ngoma Zingine Mpya Wiki Hii Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Historia imezidi kutengenezwa kwani kiwanda cha muziki nchini Tanzania kimeendelea kupokea kazi nzuri kutoka kwa wasanii wake ambao wao wana lengo moja tu, nalo ni kuburudisha mashabiki zao.

Wiki hii mambo yameendelea kuwa sukari kwani wasanii tofauti tofauti kama  wameachia ngoma na zifuatazo ni ngoma ambazo zimepamba kiwanda cha muziki Tanzania kwa wiki hii :

Wena - Jux, Khanyisa & Yumbs

Wakati tunasubiri albamu yake ya King Of Hearts iingie sokoni, Jux alisherehesha mashabiki zake na ngoma yake kali ya Wena ambayo kwa sasa inafanya vizuri sana ndani na nje ya Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=OvicQqB_QJM

Baby Boo - Mr Blue Ft Ibraah & Baddest 47

Baada ya kitambo kupita Mr Blue Byser ameamua kurudi kivingine na ngoma yake ya Baby Boo ambayo amemshirikisha Ibraah kutoka Konde Gang pamoja na Baddest 47. Humu ndani Mr Blue anahadithia ni kwa namna gani anampenda mpenzi wake huku aliweka ahadi kibao kwa mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=b7dwdPw2JuQ

Msumbufu - Balaa Mc

Utapenda namna ambavyo Balaa Mc kwenye ngoma hii ya Msumbufu amevaa uhusika wa mwanaume ambaye anamuomba mpenzi wake amrudie lakini mpenzi wake huyo haoneshi ushirikiano. Mashahiri mazuri pamoja na video iliyojaa uhalisia ndio vimechagiza ngoma hii ya Balaa Mc kuwa kali sana.

https://www.youtube.com/watch?v=5m4Vb4bh7Bc

Nifundishe - K2ga

Nyota kutokea Kings Music, wiki hii aliifundisha tasnia ya Bongo Fleva nini maana ya muziki mzuri kupitia ngoma yake nzuri ya mapenzi ya kuitwa Nifundishe ambayo imekuja miezi takriban mitano tangu staa huyo aachie wimbo wake wa Rangi Rangi.

https://www.youtube.com/watch?v=VZevDPPl_1U

Demu Wangu - Meja Kunta Ft Mabantu

Kwenye Tiktok na mitandao mingine ya kijamii ngoma inayotikisa kwa sasa ni Demu Wangu Ya kwake Meja Kunta akiwa na kundi la Mabantu. Ujumbe wa ngoma hii uliojaa vichekesho pamoja na mafunzo ya kimaisha umechagizwa mastaa mbalimbali ikiwemo Zuchu kujirekodi wakiwa wanaimba ngoma hii mitandaoni.

https://www.youtube.com/watch?v=qxUisfyokuM

Leave your comment