Nyimbo Mpya: Barnaba Aachia Rasmi Video Ya Hunitaki Akiwa Na Mbosso

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Nyota kutokea kiwanda cha Bongo Fleva, Barnaba Classic kwa mara nyingine amekidhi haja za kiburudani za mashabiki baada ya kuachia rasmi video ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu sana na mashabiko ya kuitwa Hunitaki ambayo amemshirikisha Mbosso.

Ikumbukwe kuwa Hunitaki ni video ya 3 kutoka kwenye albamu ya Barnaba Classic ya kuitwa Love Sounds Different kwani kufikia sasa Barnaba ameshaachia video ya Hadithi akiwa na Diamond Platnumz pamoja na Marry Me ambayo amemshirikisha Marioo.

Hunitaki ni video ambayo inaelezea stori ya mwanaume ambaye alijiua baada ya kushindwa kuhimili maumivu ya mapenzi yaliyotokana na kuachwa na mpenzi wake aliyekuwa akimpenda sana. Video ya Hunitaki imefanyika jijini Dar Es Salaam huku moja ya sehemu ambayo video hiyo imefanyika ni Little Theatre eneo la Masaki.

Directoe Ivan ndiye ametayarisha video hii ya Hunitaki na kando na kazi hii hii Ivan pia ametayarisha video nyingi kama Tai Chi ya Ruby Africa, Staki Mazoea Ya Shilole pamoja na Samahani ya Lulu Diva akiwa na Lavalava.

https://www.youtube.com/watch?v=HPmN1sLd-2w

Leave your comment