Nyimbo Mpya: Harmonize 'Amelowa', 'Nay wa Mitego 'Rais Wa Kitaa' Na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii
26 September 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Jumatatu ya mwisho kabisa ya mwezi Septemba imeshawadia na bila shaka wasanii mbalimbali kutoka Tanzania wameendelea kunogesha maktaba yako ya kimuziki kwa kuachia ngoma mpya na kali ambazo zina lengo la kukuburudisha na kukufurahisha pia.
Zifuatazo ni ngoma 5 mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania wiki hii :
Rais Wa Kitaa - Nay Wa Mitego
Nay Wa Mitego hatimaye ameachia albamu yake ya kuitwa "Rais Wa Kitaa" ambayo imesheheni ngoma 14 za moto.
Kupitia albamu hii Nay Wa Mitego ameshirikiana na wasanii tofauti tofauti kama Marioo, Jux, Ali Kiba, AY Master, One Six, Kelechi Africana kutokea Kenya pamoja na Runtown kutokea nchini Nigeria.
Mtoto Kaharibika - Manfongo Ft Mr Blue
Pamoja na kwamba Singeli na Hip Hop zina utofauti wa kiutamaduni lakini kupitia ngoma hii ya kwake Manfongo ya kuitwa "Mtoto Kaharibika" akiwa na Mr Blue, tofauti hizo zimewekwa pembeni.
Mdundo wa kuchezeka, mashahiri ya kuvutia pamoja na muingiliano mzuri wa sauti vimechagiza ngoma hii kuwa ya kipekee sana.
Amelowa (Video) - Harmonize
Harmonize alilazimika kwenda mpaka Upepo Beach, mitaa ya Mbezi Beach Dar Es Salaam ili kuweza kutayarisha video ya "Amelowa" ambayo kwa sasa inafanya vizuri sana nchini Tanzania.
Director Kenny ambaye ndiye ametayarisha video hii, ameonesha ufundi wa hali ya juu katika kazi hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara laki nane sitini na moja kwenye mtandao wa YouTube.
Tumekubalika Na Mungu - Ambwene Mwasonge
Wiki hii Ambwene Mwasonge ameachia wimbo wa "Tumekubalika Na Mungu" ambao kuanzia sauti, mdundo pamoja na mpangilio wa mashahiri utaweza kukubariki na kukupa faraja pindi utakapousikiliza.
Wanaongea - Dulla Makabila Ft Ngajupa
Wiki hii Dulla Makabila ameachia video yake ya "Wanaongea" ambayo imepokelewa vyema na mashabiki. Video ya ngoma hii kufikia sasa imeshatazamwa mara sitini na saba elfu kwenye mtandao wa YouTube.
Leave your comment