Barnaba Aachia Video Ya 'Mzuri', Amshirikisha Rayvanny

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania Barnaba Classic hatimaye ameachia video ya ngoma yake ya "Mzuri" ambayo amemshirikisha mwanamuziki na CEO kutokea lebo ya Next Level Music Rayvanny.

Video ya "Mzuri" inakuja ikiwa imeshatimia wiki mbili tangu Barnaba aachie video ya "Hadithi" ambayo amemshirikisha mwanamuziki kutokea WCB Wasafi wa kuitwa Diamond Platnumz, videi ambayo kwa sasa imekuwa chaguo la wengi huko Youtube.

Mzuri ni video ambayo inamuonesha Rayvanny pamoja na Barnaba Classic wakiwa wamependeza na katika mazingira mbalimbali wakiwa wamezunguka na wasichana warembo kama ambavyo mashahiri ya wimbo huo yanavyoelekeza.

Video hii imeongozwa na Eris Mzava, mtayarishaji wa video za muziki kutoka Tanzania ambaye anajulikana kwa kufanya video nyingi za mwanamuziki Rayvanny ikiwemo Siri, Te Quiero ambayo Marioo ameshirikishwa na Rayvanny pamoja na Jeniffer Remix ambayo Rayvanny alifany na Guchi kutokea huko nchini Nigeria.

Ikumbukwe kuwa hii ni video ya pili kutoka kwenye albamu ya Barnaba Classic ya kuitwa "Love Sounds Different" ambayo kwa sasa inafanya vizuri sana hapa Afrika Mashariki.

https://www.youtube.com/watch?v=xJz52_GmVYc

Leave your comment