Wasanii Watano Kutoka Tanzania Ambao Pia Ni Watangazaji

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Moja kati ya vitu ambavyo vinafanya wanamuziki wa Tanzania kuwa wa kipekee ni uwezo wao wa kufanya mambo mbalimbali kwenye tasnia nzima ya burudani na ndio maana wasanii kama Shilole, Diamond Platnumz, Rayvanny na hata Nandy ukiweka pembeni muziki, wasanii hao wanafanya biashara zao.

Kando na biashara, kuna baadhi ya wasanii kutoka Tanzania pia ni wanafanya kazi ya utangazaji kwenye redio na TV mbalimbali nchini humo. Wafuatao ni wasanii 5 kutoka Tanzania ambao pia husikika kwenya vipindi mbalimbali vya TV na Redio nchini Tanzania :

Adam Mchomvu

Ukiweka kando uwezo wake wa kipekee wa kuchana mistari lakini pia Adam Mchomvu ni fundi anayehakikisha kuwa watu wanapata taarifa za burudani zinazotakiwa kupatikana kupitia kipundi cha XXL cha Clouds FM ambacho huruka kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 10 jioni kila Jumatatu mpaka Ijumaa.

Lafudhi yake ya "Kiarusha" pamoja na utani wake kwa mtangazaji mwenzake wa kuitwa "Mamy Baby" vinamfanya kuwa bora sana awapo redioni.

https://www.youtube.com/watch?v=XAmgne1zh-A

Baba Levo

Nyimbo zake kama "Amapiano" pamoja na "Shusha" akiwa na Diamond Platnumz zimemfanya kuwa moja ya wasanii wakubwa sana Tanzania. Ukiweka kando muziki Baba Levo pia husikika kwenye kipindi cha Mgahawa cha Wasafi FM, kipindi ambacho kina mahadhi yanayoendana na "Jahazi" ya Clouds FM.

Watu wengi hupenda kumsikiliza Baba Levo kutokana na utani wake akiwa redioni pamoja na kupenda kumsifia Diamond Platnumz mara kwa mara akiwa kwenye kipindi.

https://www.youtube.com/watch?v=ph1UQR1etYQ

Frida Amani

Baada ya kufanta vizuri kwenye shindano la kusaka magwiji wa muziki yaani Bongo Star Search, Frida Amani alitimkia moja kwa moja kwenye kituo cha East Africa Radio ambapo alikuwa akishirikiana na Dullah Planet kuendesha kipindi cha Planet Bongo.

Miezi kadhaa baadae rapa huyo mwenye hit songs mbalimbali kama "Madam President" na "Imo" alipata nafasi kwenye kipindi cha XXL na Bongo Fleva ya Clouds FM.

https://www.youtube.com/watch?v=e-4KRUgR9Tg

Vanessa Mdee

Pamoja na kwamba amepoa kufanya muziki lakini mchango wa Vanessa Mdee kwenye muziki wa Bongo Fleva ni wa kiwango cha aina yake.

Vanessa Mdee ambaye kama mwanamuziki alishawahi kushinda tuzo mbalimbali kama KTMA, AFRIMA pamoja na tuzo ya Kora kama msanii bora wa kike mwaka 2016, Vanessa Mdee pia alishawahi VJ wa MTV Africa, pamoja na kuwa mtangazaji kwenye Bongo Star Search na Dume Challenge lakini pia alikuwa mtangazaji wa redio ya Choice FM kisha ya kuacha na kugeukia utangazaji.

https://www.youtube.com/watch?v=lQVIV8WJQxs

Shilole

Ukiweka kando ngoma zake kali kama "Say My Name", Shilole anajulikana kwa vitu vingi kama kuwa mpishi, mfanyabiashara, mchekeshaji, muigizaji na kubwa kabisa siku za hivi karibuni amekuwa ni mtangazaji wa kipindi cha Maskani Poa akiwa na Baba Levo, kinachorushwa Maisha Magic Poa .

https://www.youtube.com/watch?v=a4NMthVr7vc

Leave your comment