Nyimbo Mpya: 'Nikikuona' Nay wa Mitego, 'Numero Uno' ya Tommy Flavor Akimshirikisha Tanasha Dona na Nyimbo Zingine Mpya Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Bongo Fleva imeendelea kunoga na kunawiri na hii kutokana na ukweli kwamba wanamuziki kutoka Tanzania wamekuwa wakitoa ngoma mpya na kali kwa lengo la kuburudisha na kuchangamsha mashabiki zao.

Kutoka kwa wasanii kama Tommy Flavour, Ney Wa Mitego, Jay Melody na wengineo, Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka Tanzania wiki hii :

Nikikuona - Nay Wa Mitego Ft Ali Kiba

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mingi hatimaye rapa Nay Wa Mitego ameachia ngoma mpya kabisa ya mapenzi ya kuitwa "Nikikuona" ambayo amemshirikisha Ali Kiba. Huu ni wimbo ambao Nay Wa Mitego anaonesha mapenzi hadharani kwa mpenzi wake huku Ali Kiba akipamba kibao hiki kilichotayarishwa na Yogo Beats kwa ustadi mkubwa.

https://www.youtube.com/watch?v=KP7drgCU2K4

Nakupenda - Jay Melody

Baada ya kutetemesha Tanzania na "Sugar Remix" hatimaye mwandishi na msanii kutokea Tanzania Jay Melody ameachia "Nakupenda" mkwaju ambao umeundwa kwa mashahiri mazuri ya kuvutia ambayo bila shaka yatawafaa wote ambao wako kwenye mahusiano kwa sasa. Ngoma hii imetayarishwa na Jini X 66 kutoka Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=LRdmZEdZ67g

Jaro (Video) - Zuchu

Ndani ya wiki hii Zuchu alitimiza ahadi kwa mashabiki zake baada ya kuachia video ya ngoma yake ya "Jaro". Video ya "Jaro" imejaa ubunifu na upekee ambapo Zuchu anaonekana akiwa anacheza na kujiachia mbele ya mpenzi wake. Video ya "Jaro" ni video ya pili kwa Zuchu kwa mwaka huu ikiwa imeongozwa na Slowman Films kutokea Afrika Kusini.

https://www.youtube.com/watch?v=5kBlk8GsZlA

Numero Uno - Tommy Flavour Ft Tanasha Donna

Muziki wa RnB Tanzania umepata daktari wa kuitwa Tommy Flavour ambaye ameachia mkwaju wake mpya kabisa unaoitwa "Numero Uno" akiwa amemshirikisha Tanasha Donna kutokea Kenya. Numero Uno ni ngoma kali ya mapenzi ambayo Tommy na Tanasha wanasherehekea mapenzi yao kwa kusifiana na kupeana maneno mazuri.

https://www.youtube.com/watch?v=3FrrkoS_Nak

Tamu - Kusah Ft Saraphina

Namna ambavyo Kusah ameweza kupangilia mashahiri, midondoko na muingiliano wa sauti baina yake na Saraphina kwenye ngoma hii ya "Tamu" ni kitu kinachopaswa kupigiwa makofi na kila shabiki wa muziki mzuri. Ngoma hii imeweza kupokelewa vyema na mashabiki tangu kuachiwa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=AwA1f3ngcZM

Leave your comment