Nyimbo Mpya: Mauasama 'Nioneshe', 'Desh Desh' Lavalava na Nyimbo Nyingine Zilizoachiwa Wiki Hii
15 July 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo
Imekuwa ni wiki ya aina yake kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva na hii ni baada ya wasanii wakubwa kutokea Tanzania kama Nandy, Maua Sama,Lavalava, Whozu na wengineo kuachia ngoma na video kali ambazo zina lengo la kutanua maktaba yako ya muziki.
Zifuatazo ni ngoma tano kali ambazo zimeachiwa na wasanii wa Tanzania kwa wiki hii :
Nioneshe - Maua Sama Ft Ali Kiba
Hatimaye Maua Sama ameachia video ya ngoma yake ya "Nioneshe" akiwa amemshirikisha Ali Kiba, ngoma ambayo inapatikana kwenye EP ya Maua Sama ya kuitwa Cinema. Video hii imeongozwa na Director Elvis na ndani yake Maua Sama na Ali Kiba wanaonekana wakiwa wanacheza pamoja na kufurahia mahusiano yao.
Desh Desh -Lavalava
Baada ya kimya kirefu hatimaye Mwanamziki kutoka WCB Lavalava ameachia wimbo ngoma nyingine ya mapenzi “Desh Desh”. Huu ni wimbo unaongazia siri ya wapenzi wawili wanapanga kunogesha penzi lao bila ya kuwahusisha watu wengi wala mitandao. Lavalava kkwenye ufundi wake amedondosha kibao hiki hii leo na video rasmi ikitarajiwa hivi karibuni.
Sijui Nikoje - Whozu
Kwa mara nyingine tena, Whozu amedadindia kwenye wimbi la Amapiano kupitia mkwaju wake mpya wa kuitwa "Sijui Nikoje". Hii ni ngoma ambayo Whozu anakiri na kushangaa kuhusu tabia za ajabu ambazo anazo kama vile tabia ya ulevi na matumizi mabaya ya pesa. Ngoma hii imetayarishwa na S2kizzy huku maandalizi ya mwisho yakiwa yameshughulikiwa na Young Kizzy.
Napona - Nandy Ft Oxlade
Bila shaka kiu yako ya kimuziki itapona pindi utakaposikia ngoma hii mpya ya kwake Nandy akiwa na Oxlade kutokea Nigeria. "Napona" ni ngoma ya Bongo Fleva ambayo ndani yake Nandy anasherehekea mapenzi motomoto anayopewa na mwandani wake huku Oxlade akisindikiza, ujumbe wa ngoma hiyo kwa sauti yake mujarab.
Moyo - Mbosso Ft Costa Titch
Baada subira ya muda mrefu hatimaye Mbosso ameachia video ya ngoma yake ya "Moyo" ambayo imepambwa na mitindo ya kipekee ya dansi pamoja na ubunifu mkubwa. Video imeongozwa na Director Ivan kutoka Tanzania.
Bye - Billnass Ft Nandy.
Nandy na Billnass waliamua kupamba Bongo Fleva wiki hii kwa ngoma yao mpya ya kuitwa "Bye". Huu ni wimbo ambao Nandy na Billnass wanazungumzia mahusiano yao, walipotoka, changamoto walizopitia na kubwa kabisa Nandy anaweka wazi hofu yake ya kuachwa na Billnass.
Leave your comment