Mfahamu DJ Hijab, Alikosomea,changamoto anazopitia na Tuzo alizonazo

[Picha:Instagram]

Mwandishi:Branice Nafula]

Pakua Mixes za Dj Hijab ndani ya Mdundo

DJ Hijab ni nani?

Jina la usani: DJ Hijab

Jina halisi: Aisha Bakari Mohammed

Umri: 1996 (26 yrs)

Mix tapes zake ni za muziki gani: House Music, Afro house na Afrofusion

Aisha Bakari Mohammed almaarufu DJ Hijab ni mzaliwa wa Zanzibar.

Alizaliwa katika hospitali ya Mzee Abdalla Mkoani huko Pemba na akalelewa Unguja. Kwa sasa Aisha ndio DJ wa kwanza wa dini ya Kiislamu kule Zanzibar na anayecheza akiwa kwenye mavazi yake ya kidini.

Aisha anafanya kazi yake ya muziki kwa kuzingatia taratibu na miiko ya Wazanzibar ikiwemo mavazi.

DJ Hijab alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?

Dj Hijab alijifunza kufanya kazi ya kucheza santuri mwaka 2015 kupitia mtandao wa YouTube kwa kuzingatia kuwa hakuwa na fursa ya kujifunza kazi hiyo kwa Dj wenzake kwa sababu za kidini.

Kando na kucheza kwenye vilabu, DJ  pia amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio na televisheni.

Kimasomo Dj Hijab amesomea chuo kikuu cha Zanzibar alikofanya kozi ya certificate na Diploma ya teknolojia ya habari na Sayansi ya Kompyuta mwaka 2017.

Tuzo

Katika kunendesha kazi yake Aisha aliweza kupata tuzo ya woman of he Year mwaka 2019 kwenye tuzo za Women feature nchini Tanzania.

Changamoto
Katika Sanaa yake Dj Hijab anapitia changamoto mbali mbali zikiwemo za kitamaduni na kidini.

Kam binti wa uswahilini wazazi wake walitaka awe daktari lakini alijilazimu kufwata ndoto yake ya kuwa mwansanturi.

 

Leave your comment