‘Yanga Tamu’ Marioo, ‘Take One’ Country Wizzy na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii
28 February 2022
[Picha: EATV]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Kila wiki wasanii kutoka Tanzania wamekuwa wakichangamsha kiwanda cha Bongo Fleva kwa kutoa ngoma mpya kabisa ambazo zimekuwa zikiuhisha wafuasi wao.Zifuatazo ni ngoma tano kali mpya ambazo zimetikisa kiwanda cha Bongo Fleva kwa wiki hii:
Pakua nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo
Nobody - Walter Chilambo
Kwenye ‘Nobody’, Walter Chilambo anatumia kipawa cha sauti yake kusimulia ukuu wa Mungu kwenye maisha yake na namna ambavyo huruma na upendo wa mwenyezi Mungu umemzunguka.
Yanga Tamu - Marioo
Kama uliipenda ‘Bia Tamu’ kutoka kwa Marioo, basi bila shaka pia utaipenda ‘Yanga Tamu’ ambayo ni kama remix ya Amapiano hiyo. Kwenye ‘Yanga Tamu’, Marioo anaisifia sana klabu ya Yanga ambayo ni mojawapo ya klabu kubwa za soka hapa nchini Tanzania.
Tanzanite - Joh Makini
Kitu kinachovutia zaidi kwenye ‘Tanzanite’ ni namna ambavyo Joh Makini ameweza kurap kwa kiswahili lakini pia akiweka vionjo vya maneno ya kiingereza kitu ambacho kinafanya ngoma hii ambayo imetayarishwa na Switch kuweza kuwa na mzuka wa kitofauti sana.
Take One - Country Wizzy
Country Wizzy amezidi kuimarisha ufalme wake kwenye muziki wa trap kwa kuachia mkwaju wake wa ‘Take One’ ambao bila kujali umri, jinsia na ushabiki ni sahihi kusema kuwa mashahiri ya ngoma hii yanaweza kumfanya yeyote aimbe na kuruka pindi atakapoisikiliza.
The Green Light (EP) - Killy
Ukiweka kando collabo kutoka kwa wasanii kama Ibraah, Christian Bella na Harmonize kitu kingine ambacho kinafanya EP ya Killy ya kuitwa ‘The Green Light’ kuwa bora ni mpngilio mzuri wa ngoma, ubora wa sauti uliotumika ambao ni wa hali ya juu pamoja na mashairi. Hii ni EP ya kwanza kutoka kwa Killy tangu aanze muziki na pia ni EP ya tatu kuachiwa ndani ya lebo ya Konde Gang baada ya ‘Steps’ na ‘Karata Tatu’ za Ibraah kufanya vizuri.
Leave your comment