Mchango wa Serikali ya Tanzania Katika Ukuaji wa Tasnia ya Muziki

[Picha: Global TV Online]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tasnia ya muziki ya Tanzania ni moja wapo kati ya zile zilizoheshimika zaidi barani Afrika. Wasanii wa Tanzania wanaongoza katika vigezo mbali mbali ikiwemo ufuasi mitandaoni na pia kimapato. Kwa mfano, wasanii watatu wenye ufuasi mkubwa sana kwenye mtandao wa YouTube barani Afrika wanatoka Tanzania. Wasanii wa Tanzania kama vile Diamond Platnumz, Rayvanny na Harmonize wamepenya soko ya kimataifa na kuendeleza ubora wa muziki wao.

Pakua Nyimbo za Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kiwango cha ubora wa muziki wa Tanzania, hata hivyo, unachangiwa pakubwa na uungaji mkono unaopata kutoka kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Tanzania. Kwenye nakali, hii tunachambua jinsi viongozi mbali mbali, Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA) na vile vile Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imechangia kwenye mafanikio ya muziki wa Tanzania.

Uongozi wa Hayati Rais John Magufuli Pombe

Wakati wa uongozi wake, Hayati Rais Magufuli alijaribu kadri awezavyo kuleta umoja katika tasnia ya muziki. Aliwaunganisha wasanii wapinzani na kuwaleta mahasimu wa jadi kama vile Alikiba na Diamond kwenye jukwaa moja. Rais wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize hivi maajuzi alifichua kwamba hayati Rais Magufuli alimsaidia kusuluhisha matatizo baina yake na lebo yake ya zamani ya WCB. Wasanii mbali mbali walitoa nyimbo za kumsifu Magufuli wakati alikua angali hai hadi wakati wa kuondoka kwake.

Pakua Nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo

Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan

Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu, wasanii wa Tanzania kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania walipata mirabaha kwa juhudi zao kwenye muziki. Kando na Mmirabaha, Rais Samia ameonyesha ukaribu na wasanii na kuwaunga mkono katika shughuli zao za kimuziki. Kwa wakati mmoja, Rais Samia aliwapigia Nandy na Zuchu simu wakati wapo kwenye jukwaa ili kuwapongeza kwa tamasha zao.

Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA)

BASATA imehakikisha kuwa nyimbo za bongo ni zenye heshima na ubora wa kiwango cha juu. Jukumu hili limesababisha muziki wa bongo kudumu na kupazwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mara kwa mara BASATA imeingilia kati katika masuala ya nidhamu miongoni mwa wasanii wa Tanzania. Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Wasanii wengi wa Tanzania wakiwemo malkia wa muziki wa bongo Zuchu wamekiri kuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imehusika pakubwa katika kufanikasha matamasha yao. Wizara hiyo vile vile imehakikisha kuwa maslahi ya wasanii yanazingatiwa.

Leave your comment