Moni Centrozone Aeleza Sababu ya Kuachia Ngoma ya ‘Cha Mbunge’
7 February 2022
[Picha: Pinterest]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Rapa kutokea nchini Tanzania Moni Centrozone ameeleza sababu hasa zilizopelekea yeye kuachia ngoma yake yake ya ‘Cha Mbunge’ ambayo amemshirikisha msanii Kusah.
Tofauti kabisa na tulivyomzoea Moni, kwenye ‘Cha Mbunge’ rapa huyo aliimba zaidi kuhusu mapenzi na kwenye mashahiri ya ngoma hiyo, Moni anasifia uzuri alionao mpenzi wake na kuonesha, ni kwa jinsi gani amezama mapenzini na, binti huyo.
Pakua Nyimbo za Moni Centrozone Bila Malipo Kwenye Mdundo
Akiongea kwenye mahojiano hivi karibuni, Moni Centrozone alifunguka kuwa wazo la kufanya ngoma hiyo lilipatikana baada kuhisi kuwa anahitaji kufanya ngoma ya mapenzi ili kuweza kuburudisha zaidi wasikilizaji.
"Kwanza Idea imekuja kutokana na kutaka kufanya love season kufanya ngoma za mapenzi. Pia idea ilikuja kufanya ngoma na waimbaji kwa hiyo kwenye kufafuta vitu tofauti nikaona ni kitu kizuri kwangu mimi na ni kitu tofauti," alizungumza Moni.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Moni Centrozone Aachia EP Mpya ‘Road to Mazengo’
Aidha, Moni alitanabaisha kuwa kufanya kazi na Kusah lilikuwa ni wazo la muda mrefu na ndio maana hakufanya ajizi kufanya nae wimbo wa pamoja pale nafasi ilipotokea.
"Kwa mtu kama Kusah alikuwa ni mtu ambaye tulikuwa tumeplan kufanya nae kazi muda mrefu, kwa hiyo ilikuwa ni just a matter of time. Ilikuwa ni kufika muda sahihi wa kufanya kazi, kwa hiyo imetokea na ni kitu kizuri," alizungumza rapa huyo ambaye yuko chini ya lebo ya Rooftop Entertainment.
Kwa sasa, Moni Centrozone anatamba na EP yake ya kuitwa ‘Road to Mazengo EP’ ambayo imesheheni ngoma tano za moto huku akiwa amemshirikisha Young Lunya kwenye ‘Mama La Mama’, Slim Sal kwenye ‘458’ pamoja na One Six kwenye ‘Shuka la Masai’ ambayo ni ngoma namba tano kwenye EP hiyo.
Leave your comment