Killy Azungumzia ‘Ni Wewe’ Kufutwa YouTube na Ziara Yake Nchini Kenya

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo kutoka lebo ya Konde Music Worldwide Killy kwa mara ya kwanza amezungumzia suala la ngoma yake ya ‘Ni Wewe’ kufutwa kwenye mtandao wa YouTube.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, Killy alidhibitisha kuwa mtu anayefahamika kama Ian Mutisya kutoka Kenya alishtaki wimbo wake wa sababu za hatimiliki.

Pakua Ngoma za Killy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Usimamizi wake hata hivyo unafanya juu chini ili kuhakikisha ngoma hiyo inarudishwa mtandaoni.

Killy alisisitiza kuwa changamoto kama hizo ni za kawaida kwa msanii kwenye safari ya muziki. Aliongezea kuwa licha ya wimbo wake kufutwa YouTube, tayari mashabiki wako nao na wanaendelea kuusikiliza.

Kabla kufutwa kwake, ‘Ni Wewe’ ilikuwa ishatazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Video ya Killy na Harmonize 'Ni Wewe' Yafutwa YouTube

 "Kuna mtu alifanya copyright claim, akidai kuwa vionjo vya wimbo ule umefanana na vionjo vya nyimbo yake. Japo kuwa mimi kwa ufahamu wangu, ule wimbo uliimbwa na Les Wanyika, na ule mtu hahusiani na wale watu... So management wanafuatilia hilo, so ziaidi nimewaachia hiyo ni kazi yao. Lakini itarudi, very soon itarudi," Killy alisema.

Killy vile vile alizungumzia ziara yake nchini Kenya ambako yuko kwa sasa. Alieleza kuwa kilichompeleka huko ni ziara kwa vyombo vya habari ili kupanua soko ya muziki wake.

Killy ni mmoja kati ya wasanii wanaokua kwa kasi mno kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania.

Leave your comment