Video Ya Wimbo Wa 'Ni Wewe' Kutoka Kwa Killy Yachelewa Kutoka

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Maswali yameibuka miongoni mwa mashabiki wa msanii maarufu Tanzania Killy baada ya video yake iliyoratibiwa kutoka tarehe 10, Januari, 2022, kuchelewa. Killy alikua ametangaza tarehe 9, mwezi huu wa Januari kuwa ataachia video ya wimbo wake wa 'Ni Wewe' aliomshirikisha staa wa muziki wa bongo Harmonize.

'Ni Wewe' iliachiwa katika mfumo wa audio tu takriban miezi minne iliyopita. Licha ya kuwa kwenye audio bila video, ngoma hiyo ilipata mapokezi mazuri na kufikia sasa imetazamwa takriban mara milioni moja nukta saba.

Soma piaMabantu Wafunguka Jinsi Walivyompata Harmonize Kwenye "Utamu Remix"

Kwenye tangazo alilochapisha kwenye ukurasa wake wa kijamii, Killy aliwaahidi mashabiki kuwa video ya ngoma hiyo itatoka saa nne asubuhi, tarehe kumi. "Killy x Harmonize , music video tomorrow 10:00 am," Chapisho la Killy mtandaoni lilisomeka.

Takriban masaa ishirini na nne baadaye ngoma hiyo bado haijatoka licha ya kusubiriwa sana na mashabiki. Kuchelewa huko kumewafanya mashabiki kujawa na maswali, haswaa ikizingatiwa kuwa, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuelezea kisa cha video hiyo kuchelewa.

Killy hata hivyo amechapisha picha zinazoaminika kutoka kwenye video hiyo tarajiwa kwenye kurasa zake za kijamii. Harmonize kwenye ukarasa wake vile vile hajasema lolote kuhusu video hiyo ya 'Ni Wewe'. Bosi huyo wa Konde Music Worldwide amezidisha kampeni ya wimbo wake mpya kw jina la 'Serious Love'. Mashabiki wanazidi kusubiri video hiyo kutoka.

Leave your comment