Mdundo.com DJ Battle: Jinsi MaDJ wa Tanzania Wanavyoweza Kushinda Shilingi Milioni 7 za Tz

Je? Umebarikiwa na talanta ya KuDJ? Je, unatamani kupata shilingi milioni saba za Tanzania? Basi jaribu bahati yako kwenye shindano ya Mdundo.com DJ Battle.

Mdundo.com DJ Battle ni Nini?

2021 Mdundo.com DJ Battle ni shindano la maDJ. Shindano hili lilianza nchini Tanzania siku ya Ijumaa, tarehe 19 Novemba, 2021. Shindano hilo litakalodumu kwa wiki 4, litamshuhudia DJ mmoja akitawazwa ‘King of The Turntable.’

Mshindi atakabidhiwa mkataba wa udhamini wenye thamani ya Tsh 7,000,000. Mixtape ya atakeyeshinda itapata kuchezwa kwenye redio na pia kwenye hafla kubwa ya muziki.

Ni Nani Anayestahiki?

Shindano liko wazi kwa DJs wote. Aina yoyote ya muziki inaweza kuingia kwenye shindano, iwe ni Afropop, Bongo flava,Singeli, Amapiano, Hiphop, Gospel...na kadhalika

Jinsi ya kujisajili?

Tembelea mdundodjbattle.com ili kujiandikisha na kuanza kupakia mchanganyiko.

Leave your comment