Nikki Mbishi, Songa na One The Incredible Waandaa Ziara ya Muziki Pamoja!
4 February 2015
Licha ya kutangaza kuachana na muziki, Nikki Mbishi amesema anakuja na tour ya muziki atakayokuwa pamoja na Songa na One The Incredible.

Nikki Mbishi, One The Incredible na Songa (Mwisho Kulia)
Nikki ameiambia blog ya Tanzania, Bongo5, kuwa ziara hiyo haitotegemea matangazo makubwa ila wao wenyewe watatumia nguvu zao ili kuwafikia mashabiki wa muziki wao.
“Binafsi kipo kitu nimekipanga ambacho ni tour ambayo itakuja nitakuwa na Songa, Stereo, nitakuwa na One pengine ndo muda pekee ambao mimi nitakutana nao tena na kuzungumza nao yale yaliyonisibu katika ile hali ambayo tunaitengeneza kutaka kupeleka muziki kule tunapotaka uende,” amesema Nikki.
“Itakuwa sio busara kuwapachikia mangoma kibao ya zamani na sisi sidhani tena tunahitaji radio kwaajili ya kusikika. Sisi hatuna muda huo. Sasa hivi tunafanya jitihada za kufikisha nyimbo zetu kwa watu bila kuingiliwa na mtu, sio mpaka radio au TV au uende wapi. Watu wanaweza wakaweka ngoma mtandaoni tu na zikawafikia watu wetu. Kutoa ngoma muziki ni maisha yangu mimi. Mimi ninaweza nikauchukua muziki wangu niliourekodi 2005 wewe haujui, nikaamua kuuweka Mkito, wakasema Nikki Mbishi katoa wimbo mpya lakini sio ngoma mpya. Mimi naachia mangoma kibao ambayo yapo niliyarekodi zamani, sisemi kwamba nitatangaza kwamba watu wawe attention Nikki anarudi no,” ameongeza rapper huyo.
Ungependa pia kusoma
Radio and Weasel Watoa Video Mpya!
Kwa upande mwingine, Nikki Mbishi amesema baada ya kutangaza kuachana na muziki, ametambua ana umuhimu gani katika muziki wa Hip Hop Tanzania.
“Kwa haraka haraka hii ni namna ya kutafuta takwimu watu wangapi wapo pamoja na wewe kwahiyo mara nyingine ili upate kusikika na watu kwa kile unachokifanya ni lazima utafute usikivu kwanza. utayari wa watu hao kukusikiliza. Kwahiyo mimi nilijaribu kuangalia OK nafanya hii kazi najifurahisha? Je hawa watu wanakithamini ninachokifanya? Kwahiyo hiyo kwa namna moja ama nyingine inaweza ikani-motivate mimi ikanipa mimi ari nyingine ya kusema hapana kumbe bado uwezo ninao, kwa sababu watu wamekubali kile ninachokifanya.”
Original Story courtesy of Bongo5
Contibution: PETER N Digital Media, Mdundo.com




Leave your comment