Seneta Kilaka Aachia EP Yake Mpya ‘King of Singeli’

[Picha: Side Makini]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Seneta Kilaka ameachia EP yake mpya kabisa inayoitwa ‘King Of Singeli’.

Seneta Kilaka ni mojawapo ya wasanii wa Singeli waliovutia sana watanzania kwa kipindi cha hivi karibuni. Senata Kilaka alipata umaarufu zaidi baada ya mwanamuziki Hamisa Mobeto kufanya remix ya wimbo wake wa ‘Ex Wangu’.

Soma Pia:Meja Kunta Atangaza Ujio wa EP Yake Mpya

EP ya Seneta Kilaka imesheheni ngoma nne za moto ambazo ni ‘Ninae Share Nae’, ‘Nyota’, ‘Ninavyopendwa’ pamoja na ‘Tabasamu Lako’.

Kinacholeta bashasha zaidi kwenye kazi hii ni kuwa Seneta hajashirikisha msanii yeyote bali amefanya EP yote pekee yake.

Ufundi mkubwa wa kimashairi yanayogusia mambo mbalimbali ya kimaisha pamoja na mdundo mujarab uliopikwa na kupikika kutoka kwa Jay Stereo umefanya kazi hii ya Seneta Kilaka kuwa yenye hadhi ya nyota tano.

Soma Pia: Jay Melody Azungumzia Ripoti Kuwa Amejiunga na Lebo ya Rayvanny Next Level Music

Aidha, kwenye mahijiano aliyoyafanya hivi karibuni Wasafi FM, Seneta Kilaka amedokeza kuwa kwa sasa chini ya usimamizi wa Mobetto Music ambayo ni lebo iko chini ya Hamisa Mobetto.

Kando na EP hii, Seneta Kilaka ameshatoa mikwaju mingi iliyofanya vizuri nchini Tanzania kama vile ‘Usije Ukazima’, ‘Simwachi’, ‘Zoa Zoa’, ‘X Wangu’ na nyinginezo nyingi.

Leave your comment