Historia ya WAKURYA

KABILA LA WAKURYA. #01
Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya.
Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao ni Kikuria.
Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji.
Kilimo cha asili walikuwa wanalima ulezi mtama na viazi tu kwa ajili ya kutengeneza Togwa (obosara) na Pombe. Mazao mengine yalianza kulimwa miaka ya 1900 baada ya wajerumani kuhimiza kilimo. Wakurya hawapendi kutawaliwa wala kuonewa hivyo walikuwa na saiga lika ya vijana kwa ajili ya ulinzi na usalama hivyo utumwa haukuwaathiri sana. Ila kwa kupenda kwao vita walijiunga sana na jeshi K.A.R (King African Rifle) kupigana vita ya kwanza na ya pili na ya Uganda.
Wakurya ndilo kabila ambalo huona vita kama Mchezo na kuua wakati wa vita ni kama kucheza tu na usiombe ukutane nao wakiwa na hasira. Ila ni watu wema sana wakati wa amani usipowachokoza hawana ubaya na MTU ila ukiwakosea bila kujua hukusamehe hats kabla hujaomba msamaha ila ukiwakosea makusudi hawana msamaha kabisa. Wakurya ni watu ambao hawasalimu amri ukionesha kuwashinda huenda kujipanga upya na kutafakari ni jinsi gani watashinda na si watu wa kukata tamaa na wakiwa na mori hawaogopi chochote wala lolote wako tayari kukabiliana nalo.
Hasa Abakuria walio katika wilaya ya Serengeti wanatambulika kama wafugaji.
Abakuria wanafanana na Wakisii wa nchini Kenya kwa lugha na umbile. Wanadhaniwa walikuwa kundi moja hadi waliposhambuliwa vikali na Wamasai mnamo karne ya 19 na kusambaratishwa katika maeneo tofautitofauti. Lakini kuna lika ambalo liliandaliwa likapewa mafunzo ya kivita ili kukabiliana na wamasai kwa kutumia pinde na mishale ambapo waliwafuata wamasai na kuwaua kwa wingi ndipo ukawa mwisho wa vita kati ya wamasai na wakurya pia eneo la mbuga ya serengeti na masai mara likapatikana baada ya wamasai kufukuzwa hadi arusha. Ndipo wakurya wakaweka makao yao ya kudumu eneo hilo na kuendesha Shughuli ya ufugaji na kilimo.
Utengano huo ulisababisha kuweko kwa lahaja mbili ambazo zinaeleweka na kila kundi.
Wakurya ni watu wenye upendo sana wakati wa amani hukubali kukaa na wageni na kuchukuliana kama ndugu, na hii ilipelekea kuwepo wakulya wenyeasili ya makabila jirani mfano kuna wakurya wenye asili ya wajaluo, wasukuma, wamasai n.k.
Abakuria wamegawanyika katika "makabila madogo" au koo kumi na sita, nazo ni:
Nyabasi,
Bakira,
Bairege,
Bagumbe (wanaoishi katika wilaya za nchini Kenya na Tanzania),
Batimbaru,
Banyamongo,
Bakenye,
Basimbiti,
Basweta,
Barenchoka,
Baikoma,
Bamerani na mengineyo.
Makabila haya madogo yote yapo pia katika kabila la Wakisii nchini Kenya.

Inaendelea.......

Leave your comment