Nyimbo Mpya: Barakah The Prince Aachia ‘Mazima’ [Video]

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maaraufu kutoka Tanzania Barakah The Prince ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Mazima’.

Tofauti na wimbo wake wa ‘Yanachosha’, kwenye kibao hiki Barakah anaonesha furaha yake kwenye mapenzi dhahiri shahiri na anamshukuru mpenzi wake kwa kumpa mapenzi motomoto ambayo hapati sehemu yoyote ile.

"Hukujali nimekufanyia mangapi nikakukosea na bado na bado ukanikumbatia furaha yangu hukuiondoa hivi nilipe nini kitakachogharamia thamani ya mapenzi yako kwangu," anaimba Barakah The Prince kwenye wimbo huu.

Utamu wa wimbo huu unatokana na ukweli kuwa umetayarishwa na manguli wawili wa muziki ambao ni mtayarishaji chipukizi Smart Junior Wonder pamoja na Abydady ambaye pia ameshiriki kutayarisha wimbo wa ‘Nidonoe’ wa Rich Mavoko.

Kabla ya wimbo huu, Barakah The Prince aliachia wimbo wake wa ‘Rainey’ mara tu baada ya kutangaza kuingia mkataba na kampuni ya Skyfye na kabla ya hapo Barakah aliitetemesha Tanzania na wimbo wake wa ‘Yanachosha’ ambao ulifanya vizuri sana.

Aidha,Barakah The Prince amesindikiza wimbo huu wa ‘Mazima’ na video ambayo imeongozwa na Director Jordan Hoechlin ambaye pia alihusika kwenye video za wasanii kadhaa kutokea Tanzania kama ‘Mapopo’ ya Damian Soul pamoja na ‘I do’ ya Winnie na Darassa.

https://www.youtube.com/watch?v=dx9FpQAxkqo

Leave your comment