Eid Al Adha : Pakua Mixes Kali Unaposheherekea Eid Al Adha 2021
20 July 2021
[Picha: Mdundo]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Eid Al Adha imeshagonga hodi na bila shaka waumini wa dini ya kiislamu wameshaifungulia milango. Kwa mwaka 2021 siku kuu hii adhimu inaadhimishwa na waislamu duniani kote kuanzia jioni ya Jumatatu ya tarehe 19 Julai na itaendelea mpaka Jumanne ya tarehe 20 Julai.
Sikukuu ya Eid Al Adha ina maana kubwa sana kwa waumini ya dini ya kiislamu kwani inakumbusha jinsi ambavyo Baba wa Imani Ibrahim alivyodhamiria kumtoa sadaka mwanae Ismail ili kutiii agizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Hivyo basi katika sikukuu hii waislamu, aghalabu huchinja wanyama wanaofaa kuliwa na kugawa nyama hiyo kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na watu maskini.
Makala hii imelenga kuangazia Mixes kali kutokea hapa Mdundo zilizotengenezwa makhususi kuisindikiza sikukuu ya Eid Al Adha na ambazo unaweza kusikiliza na kupakua bure kabisa:
Tushangilie Eid Special
Hii ni mix ya kipekee sana ambayo imesheheni nyimbo za kuabudu pamoja na Kumsifu Allah. Aidha Mix hii inawakumbusha waislamu kufanya matendo mema kipindi cha Eid kama vile kupeana zawadi, kuwavika watoto nguo nzuri na kuombeana mema. Nyimbo zilizounda mix hii ni pamoja na "Ya Rasullah" iliyofanywa na Bin Zakir, "Tushangilie Eid Abkhelef" ya Abkhelef, "Metamani" ya Muhamad Mbinda pamoja na "Muhibu" ya Mafta.
Eid Mubarak: Special Mix 2
Special mix 2 ina upekee wake kwani imesheheni wasanii tofauti tofauti ambao kupitia nyimbo zao wanamuomba Mwenyezi Mungu msamaha kwa dhambi ambazo wamezifanya lakini vile vile inawakumbusha waislamu umuhimu wa kusaka elimu ya dini ya kiislamu ili kustawisha imani yao na kufuata ambayo Mtume Muhamad aliyafundisha.
Mix hii ambayo inapatikana bure hapa Mdundo na imesheheni nyimbo nyingi ikiwemo "Tawbar" ya kwake Bin Zakir, "Tusake Elimu" ya kwake Yahya Ally, "Sifa za Rasul" ya Mwanamiraji Mwinjuma na wimbo wa kwake Fadhil Omar unaokwenda kwa jina la "Mashaallah".
Eid Mubarak: Special Mix
Kwa wale ambao wako kwenye mahusiano basi hii ni kwa ajili yenu, kwani Mix hii imesheheni nyimbo za mapenzi ambapo wasanii wamesifia wapenzi wao na kuwakumbusha kufuata misingi ya dini ya kiislamu ili ndoa zao zistawi. Baadhi ya nyimbo kali zilizomo kwenye mix hii ni pamoja na "Mashaallah" ya Fadhila Omar , "Taubatan" ya kwake Knockout Music, "Mama Amina" ya Abkhelef Music na wimbo wa " Ramadhan Bin Assad"
Inna lillah: Eid Special
Kwa wale ambao wanapitia kipindi kigumu kwenye maisha yao basi Mix hii itawahusu sana, kwani imehusisha nyimbo ambazo zinatoa faraja na tumaini pale ambapo binadamu anapitia magumu kama ugomvi kwenye familia, misiba ya ndugu na jamaa na changamoto nyingine. Audha Mix hii inawasihi binadamu kumcha Mungu na kumtumaini yeye. Baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye mix hii ni pamoja na wimbo wa Yahya Ally "Innaillah", " Naumia" wa Raudha Kids, "Idul Fitri" wa Ida Laila pamoja na wimbobwa Fadhila Omary uitwao "Utaulizwa"
Leave your comment