Nyimbo Mpya: Killy Aachia Wimbo Mpya ‘Mwisho’ [Video]

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea label ya Konde Music Worldwide Killy ameendelea kuporomosha burudani kali kwa mashabiki kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘Mwisho’.

Killy ambaye anasifika kwa uandishi wake mzuri ameachia wimbo huo ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu alipotoa ‘Roho’; wimbo ambao umeweza kufanya vizuri kwenye chati mbali mbali za muziki nchini Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Beka Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘In Love’ na ‘Umerogwa’

‘Mwisho’ ni wimbo wenye vionjo vya bongo fleva na kwenye wimbo huu Killy amevaa uhusika wa mwanaume anayeteswa kimapenzi na mwanamke wake. Hivyo anaona ni bora mahusiano hayo yafike mwisho.

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huo, Killy analalamika namna ambavyo mpenzi wake sio mwaminifu akiimba.

"Ukweli mama unauficha tena unaniruka kando usijitetee, ajali kila kukicha ex wako yanamtoka mafumbo ili unipotee," aliimba Killy.

Anaendelea kwenye aya ya pili akiimba "Maumivu moyo wangu una maumivu kidonda, mwili umepatwa na uvivu penzi limegeuka majivu nahisi kukonda."

Soma Pia: Lulu Diva Amsifu Zuchu Kwa Kuwa Moja wa Wasanii Bora Tanzania

Killy ni mojawapo ya wasanii ambao ni wazuri sana kwenye kuandika nyimbo zinazogusa hisia za watu walioumizwa na mapenzi. Kando na wimbo huu, nyimbo kama ‘Rudi’, ‘Roho’, ‘Nikwambie’ pamoja na ‘Gubu’ akimshirikisha Alikiba zinaonesha ni kwa vipi Killy ni mzuri kwenye eneo hilo.

Kabla ya kuingia kwenye label ya Konde Music Worldwide, Killy alikuwa chini ya Kings' Music label iliyoko chini ya Alikiba na wimbo huu ni wimbo wa pili tangu Killy ajiunge na Konde Music Worldwide.

https://www.youtube.com/watch?v=1jag9EhRvkk&ab_channel=Officialkilly

Leave your comment