Guchi Atangaza Ujio wa Video ya ‘Jennifer Remix’ Akimshirikisha Rayvanny

[Picha: Guchi Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Nigeria Guchi ametangaza rasmi kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ujio wa video ya ‘Jennifer Remix’ akimshirikisha Rayvanny.

Soma Pia: Msanii Guchi Kutokea Nigeria Azungumzia Kufananishwa na Zuchu

Guchi alisafiri kwenda Tanzania siku chache zilizopita ambapo amekuwa akishughulikia utengenezaji wa video ya wimbo huo.

Katika tangazo ambalo alichapisha kwenye mtandao wa Instagram, Guchi aliwauliza mashabiki wake ikiwa wako tayari kwa video hiyo kutolewa. Aliambatanisha ujumbe huo na picha ambayo ilimuonyesha akiwa pamoja na Rayvanny.

Soma Pia: Rayvanny, Guchi Waanza Harakati za Kuachia Video ya ‘Jenniffer Remix’

Picha hiyo inaonekana kutoka kwa video ya Jennifer remix inayotarajiwa. Rayvanny alitoa maoni yake kwenye chapisho hilo la Guchu na kuonekana mwingi wa hamu ya kuachia video hiyo.

"Are you ready for this? Guchi X @rayvanny #jenniferremix," Guchi aliandika katika mtandao wa kijamii.

Kwa upande mwingine Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram alidai kwamba anahitaji maoni 5,000 kwenye chapisho lake la mtandao wa kijamii kisha video hiyo itatolewa.

"#CHUI X @officialguchi 5000 comments we drop it let’s go," chapisho la Rayvanny lilisoma.

Hakuna hata mmoja wa wanamuziki hao aliyedokeza tarehe au saa halisi ambayo video hiyo itatolewa. Awali Rayvanny alifunua kuwa Guchi atakuwa akifanya kazi kwenye miradi kadhaa ya muziki naye. Guchi pia alionyesha nia ya kufanya kazi na wanamuziki wengine wa Tanzania akiwemo Zuchu.

Leave your comment