Msanii Guchi Kutokea Nigeria Azungumzia Kufananishwa na Zuchu

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Guchi kutoka nchini Nigeria ameweka wazi anavyojisikia pale ambapo watu wanamfananisha na msanii Zuchu kutokea label ya WCB. Guchi aliingia nchini Tanzania siku chache zilizopita na kukaribishwa na mwenyeji wake Rayvanny.

Akiwa kwenye mahojiano, alieleza kuwa sio kitu kibaya kufananishwa na Zuchu kwani wote ni wasanii. Guchi alisema "Zuchu ni Zuchu. Mimi ni Guchi tumetokea nchi mbili tofauti na namkubali Zuchu na sioni ubaya wowote kufananishwa nae."

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

Guchi aliongeza kwa kusema kuwa alimfahamu vizuri Zuchu baada ya kusikia wimbo wake wa ‘Sukari’ uliotoka Januari mwaka huu na toka hapo akavutiwa na kazi za msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Nyumba Ndogo’.

"Nilimfahamu Zuchu mwaka huu kwa wimbo wake wa Sukari na niliposikia wimbo ule nikapenda muziki wake. Nilimfahamu Zuchu nikiwa tayari nishatoa EP yangu ya Iam Guchi" aliongeza msanii huyo ambaye anatamba na wimbo wake wa Jeniffer Remix aliomshirikisha Rayvanny.

Sambamba na hilo, kwenye mahojiano hayo Guchi aliweka wazi kuwa wanaigeria wanaukubali sana muziki wa Bongo Fleva na kwamba Rayvanny na Diamond nyimbo zao zinazisikilizwa sana huko Nigeria.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

"Wanaigeria wanapenda muziki wa Bongo Fleva, kila mara unasikia watu kama Diamond Platnumz nyimbo zao zinachezwa kwenye vituo kama Soundcity, MTV base pamoja na HipTv," alisema msanii huyo.

Kwa sasa, Guchi yuko nchini Tanzania na alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya Next Level Music ya Rayvanny. Msanii huyo amedokeza kuwa kuwa kuna nyimbo nyingi nzuri ameshafanya na msanii Rayvanny kutokea WCB.

Leave your comment