Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Ngoma Mpya ‘Nikomeshe’

[Picha: Lava lava Instagram]

Mwandishi: Charles maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Lava Lava ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Nikomeshe’.

Kwenye wimbo huu, Lava lava ambaye ni msanii kutokea lebo ya WCB anaelezea jinsi mapenzi yanavyomtesa na kumfanya apate sonona.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video Rasmi ya 'Nyumba Ndogo'

Lava lava kwenye kiitikio cha wimbo huu anasema "Nikomeshe malipo duniani yote ni mapito. Nikomeshe kila lenye mwanzo halikosi mwisho. Nikomeshe jua kila mtihani una suluhisho. Nikomeshe nione hamnazo fungu langu liko."

Kwenye ubeti wa pili wa wimbo huu Lava lava anaonesha jinsi hali ya kuachwa inavyomfanya awe na sonona. "Sonona sono, penzi kalikatisha, sonona sono mwambieni japo awe na imani, sonona sono mi mwenzake nitapendwa na nani?"

Mashabiki wengi wamekuwa na hisia tofauti tofauti baada ya wimbo huu kutoka huku wengi wao wakimpa pole Mr Love Bite baada ya kuachwa hadharani na mpenzi wake Lulu Diva kwenye kipindi cha Redio cha Lavidavi cha Diva The Boss.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

Kwenye akaunti ya YouTube ya Lava lava, wengi walitoa maoni yao kuhusiana na wimbo huu kuna mchangiaji mmoja aliandika "Stay strong. I know how you feel". Mwingine aliandika "Sema freshi kazi nzuri huyo achana nae kama hataki kuelewa pendo lako".

Bado video ya wimbo huu uliofanyiwa maandalizi ya mwisho na Mix Killer haijatoka na mpaka sasa Lava lava hajaweka chapisho lolote linalohusiana na wimbo huu kwenye akaunti yake ya Instagram.

Lavalala alijiunga na WCB mwaka 2015 na kutambulishwa rasmi kama msanii wa label hiyo mwaka 2017 baada ya kutoa wimbo wake ‘Tuachane’.

Tokea hapo, Lava lava amekuwa ni msanii asiyeachwa kuongelewa midomoni mwa watu kwani amekua akitoa nyimbo kali kama Saula, Habibi, Nitake Nini, Go gaga, Bado Sana na mwezi Februari aliachia EP yake iitwayo Promise EP akiwashirikisha bosi wake Diamond Platnumz na Mbosso.

https://www.youtube.com/watch?v=m0fEkdKfh3c

Leave your comment