Man Fongo Ahimiza Watanzania Kutomkejeli Diamond kwa Kukosa BET

[Picha: Man Fongo Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Singeli Man Fongo amewahimiza Watanzania kutomkejeli Diamond Platnumz baada ya kukosa tuzo la BET. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Man Fongo alisema kuwa suala la Diamond kupata uteuzi kwenye tuzo hizo za BET ni suala kubwa sana hata kama hajashinda.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

"Leo hii Diamond sio kwenda kule kukosa ile tuzo ndo kashindwa kabisa katika muziki ila ina maana katika muziki wetu sisi watanzania kuna mtu kaenda kutuonesha kitu ambacho inabidi tukipambanie. Wote tuwe na nguvu tushikane tuweze kuwa kitu kimoja," Man Fongo alisema.

Man Fongo aliongeza kuwa Diamond Platnumz anajitahidi sana kuupeleka mbele muziki wa Tanzania ila kuna baadhi ya watu wanamrudisha nyuma.

Kwa sasa Man Fongo ameachia EP yake inayokwenda kwa jina la ‘Ndio basi tena’. EP hii imemfanya Man Fongo  kuwa msanii wa kwanza wa singeli kutoa EP.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

EP hiyo imesheheni nyimbo 5 kama ‘Ndo basi tena’ akimshirikisha Stamina, ‘Kama Vocha’ akimshirikisha Machupa, ‘Spesho’, ‘Rudi’ na ‘Hainogi’.

Aidha kwenye mahojiano aliyoyafanya kwenye kipindi cha XXL, Man Fongo alieleza kuwa Shilole ndiye msanii ambaye amemsaidia sana kumpa ‘michongo’ tofauti tofauti.

"Yaani katika safari yangu mpaka nafika hapa namiliki gari sijui najenga, madili mengi amenipa shishi (Shilole). (Shilole) huniambia Man Fongo nakupa hili dili na ole wako usijenge. Mimi hadi leo sijamalizia nyumba na nina ugomvi nae," Man Fongo alisema.

Leave your comment