Ruby Aelezea Chapisho Lake Instagram Kuhusu Kuacha Muziki

[Picha: Classic 105]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Hellen Majeshi almaarufu kama Ruby Africa hivi majuzi aliteka hisia za mashabiki zake baada ya kuchapisha picha kwenye akaunti yake ya Instagram yenye maneno "Mara Paap! Ruby kaacha muziki".

Chapisho hilo lilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo mashabiki wa msanii huyo walihisi kuwa Ruby yupo mbioni kuacha muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

Akiongea kwenye kipindi cha The Switch, Ruby ameeleza kiundani kuhusu chapisho hilo. Ruby alisema "Ukimuna kobe kainama ujue anatunga sheria lakini sio kama nimeacha muziki ama vipi, mtakuja kujua nimeacha ama inakuaje lakini hayo mengine ni mawazo tu ya hapa na pale."

Kupitia mahojiano hayo pia Ruby alisema kuwa kwa sasa yuko kimya kwa sababu kuna kazi nyingi anaziandaa kwa ajili ya mashabiki zake. "Nina kazi nyingi sana za kuandaa na tayari zipo its just mipango ya muda na kuachia tu lakini kazi zimejaa tele, zipo za kutosha."

Ruby aliachia wimbo wake wa mwisho uitwao ‘Wanakoma’ Machi mwaka huu na tangu hapo amekuwa kimya.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Ruby aliingia rasmi kwenye tasnia ya muziki mwaka 2014 baada ya kuibuka kidedea kwenye shindano liitwalo Serengeti Fiesta Super Nyota Diva lililoandaliwa na Clouds Media pamoja na Primetime promotions.

Baada ya kushinda shindano hilo, Ruby akawa chini ya Tanzania House of Talents (THT) na akatoa wimbo wake wa kwanza uitwao ‘Na Yule’ wimbo alioandikiwa na msanii Barnaba kama zawadi ya kushinda Super Nyota Diva.

Wimbo wa ‘Na Yule’ ulimfanya Ruby kufahamika Tanzania nzima na tokea hapo akapata nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha makubwa kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards, Zanzibar International Film Festival (ZIFF) 2015, Uzinduzi wa kampeni za Urais Zanzibar na Coke Studio Sessions akishirikiana na wasanii wakubwa barani Afrika kama Yemi Alade.

Mpaka sasa, Ruby hajaachia albamu yoyote lakini ametoa nyimbo nyingi kama vile ‘Wamekoma’, ‘Alele’, ‘Yako Wapi Mapenzi’, ‘Niwaze’, ‘Sijutii’ na nyinginezo kibao.

Leave your comment