Diamond Platnumz Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz ametangaza kuwa anakwenda kuachia wimbo mpya hivi karibuni. Diamond Platnumz aliingia kwenye mitandao ya kijamii ambapo alitangaza habari hiyo.

Wakati akitangaza habari hiyo, Diamond alichapisha video iliyopita ambayo ilimuonyesha wakati akiburudisha mashabiki wake. Nyota huyo hakutoa maelezo zaidi juu ya wimbo huo na aliwaacha mashabiki wake wakiwa na hamu.

Soma Pia: Lava Lava ft Mbosso 'Basi Tu': Nyimbo Mpya Tanzania [Video]

Habari hizo zilipokelewa vyema miongoni mwa mashabiki wake huku wengi wakimtaka kuarikisha na kuutoa wimbo huo.

Huu utakuwa wimbo wa kwanza ambao Diamond ataachia baada ya kuwa kimya kwa nusu mwaka. Wimbo wa mwisho ambao Diamond alitoa ni "Waaah" ambapo alishirikiana na mwanamuziki wa Kongo Kofi Olomide.

Wimbo huo ulifanya vizuri na hadi sasa umepata mamilioni ya watazamaji kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

Mradi mpya wa Diamond unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi ikizingatiwa kwamba utakuwa wimbo wa kwanza ambao ataachia chini ya usimamizi wa Warner Music Group. Warner Music Group ambalo ni moja ya lebo kuu za rekodi za muziki za kimataifa lilisaini Diamond hivi karibuni.

Tofauti na hapo awali ambapo lebo ya WCB ndiyo ilikuwa inashughulika na uandalizi wa ngoma zake Diamond, kazi hii mpya itafanywa na kampuni ya Warner Music.

Leave your comment