H baba: Diamond Platnumz ni Mchokozi, Anatumia Muziki Kuwakejeli Wasanii

[Picha: Hulkshare]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa mziki wa Rhumba kutoka Tanzania H baba amejitokeza kuzungumzia uhasama ulioko kati yake na wasanii wa WCB kwa jumla. Kwa muda mrefu, H baba hujichukulia jukumu ‘Kumkosoa’ Diamond Platnumz haswa katika kazi zake kimziki.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Katika kutaka kujua uhalisia wa hisia za H baba kwa timu nzima ya WCB, H baba alifunguka katika mahojiano na mwanahabari wa Wasafi media ambapo alimtuhumu Diamond kama mtu mchokozi.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea Leo Usiku

Kwanza alianza kwa kukana kuwa yeye hamchukii Diamond Platnumz. Alipoulizwa mbona anapenda kumchokoza Diamond Platnumz, alisema kuwa Diamond ndiye alianza kumchokoza yeye kwa kutumia msanii wake Mbosso kwa kusema “Maunao ya H baba ni zilipendwa”.

“Watu wanauliza nani mchokozi. Diamond alichukua vijana wake, wakatengeneza nyimbo na kuniimba kuwa uno la H baba ni zilipendwa, sasa apo nani mchokozi?” aliuliza H baba.

Vile vile, H baba alidai kuwa Diamond Platnumz na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu ndio walianzisha vikundi katika mziki wa Tanzania, jambo ambalo yeye anapinga kwa sana.

 “Ni yeye na wema ndio walianzisha hizi timu na mimi kwanza nilikua mtu wa kwanza kukataa hii timu na pia niliendelea kutukanwa, naamini kwamba hizi timu zitamgeuka yeye sababu binaadamu hana shukrani…..mimi naamini timu zisingekuwepo mziki wa Tanzania ungekuwa mbali sana. Ndio maana Konde gang hakuna timu, Konde gang ni family…” alisema H baba.

https://www.youtube.com/watch?v=dpFpApiQ5dk

Leave your comment