Nyimbo Mpya: Baba Levo Aachia Ngoma Mpya’ Amapiano’ Akimshirikisha Oti

[Picha: Babalevo Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii na mtangazaji Babalevo ameachia kazi yake mpya kwa jina “Amapiano.”

Huu ni wimbo wenye maudhui ya densi huku ukibeba ule mdundo wa Afrika kusini Amapiano ukichanganywa na biti za kiarabu arabu hivi.

‘Amapiano’ ni mdundo unaondelea kupata umaarufu Afrika Mashariki na kazi hii ni dhihirisho kuwa wasanii wa Tanzania pia wameudakia mdundo huu kwa faida yao.

Soma Pia: Rayvanny vs Harmonize: Baba Levo Atozwa faini ya Tsh Milioni Moja Baada ya Kutoa Mwimbo Chafu.

Katika wimbo huu Babablevo amemshirikisha msanii wake Oti ambaye anaendelea kukua kwa kasi katika sanaa yake.

“Washikaji waonyeshe michongo, waonyeshe manjia, kasha cheza kiminyato, ama chezo kimikato,cheza kama battle,vua mpaka na viatu….” Aliimba Babalevo.

Wimbo huu ni mzuri kwa tamasha za mziki na hata sherehe tofauti tofauti. Wimbo huu umetengezwa na mwandalizi mziki Bob Junior na kufanyiwa mchanganyiko na producer Mocco Genius.

SOMA PIA: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Kwa upande wake, Oti hajaachwa nyuma alivyodondosha mistari yake kwa ufundi mkubwa. Hivyo sasa mashabiki wamerukia wimbo huu kuifanyia #challenge ya kudensi ili kuusambaza mziki huu.

Vile vile mashabiki wanatarajia kanda ya wimbo huu hivi karibuni. Kufikia sasa, wimbo huu unaendelea kupata umaarufu zaidi kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya elfu thelathini.

https://www.youtube.com/watch?v=r_68LbiFs5U

Leave your comment