Dulla Makabila Aachia Wimbo Mpya wa Singeli “Simanzi”

(image source:Youtube)

By Branice Nafula

Msanii tajika wa mziki aina ya Singeli Dulla Makabila amaeachia wimbo wake mpya kwa jina “Simanzi”.

Hii ikiwa njia yake ya kipekee ya kumuomboleza aliyekuwa rais wa Muungano wa Tanzania Hayati Daktari John Pombe Magufuli. Mafufuli alifariki hivi karibuni kwa ugonjwa wa moyo.
“Simanzi” ni wimbo wenye hisia nzito za machungu ambapo Dulla anaangazia kifo cha rais huyo aliyekuwa mpiganiaji wa haki na alaipendwa na wengi.

Join Us on Telegram

“Mwili ushakufa ganzi anagalia taifa nzima simanzi, wafanyakazi na wanafunzi wanalia umetutoka kipenzi, Baaaaaaba umetuacha wanao…” aliimba Dulla.
Dulla Makabila anamuangazia Magufuli kama shujaa wa Afrika kwa kazi aliyoifanyia Tanzania.
Kanda ya wimbo huu ilitengezwa kwwa ufundi na pia haikua na kazi nyingi. Ilitengezwa ndani ya studio na kufanyiwa uhariri mzuri wa kuonyesha hisia walizonazo Watanzania na hata Makabila mwenyewe.

Hii ni mojawapo tu ya baadhi ya nyimbo zilitungwa na wasanii wa nchi hiyo. Makabila kuitumia singeli imeonyesha utofauti kwa mziki huu wa singeli pia ni kigezo kikubwa katika fani ya mziki humo nchini.

Bali ameufanya wimbo huu kwa kasi ya chini kiasi mdundo wa singeli ni dhahiri. Kufiki sasa wimbo huu unaendelea kupokelewa vizuri na mashabiki kwenye mtandao wa YouTube. Dulla Makabila ni mmoja wa wasanii wanaotarajiwa kuimba katika hafla nzima ya safari ya mwisho ya Hayati Magufuli nyumbani kwake Chato atakapozikwa rais huyo.

Download Diamond Platnumz Music FREE

https://www.youtube.com/watch?v=ki_u-tpyUis&ab_channel=DullaMakabila

 

Leave your comment