Nyimbo za Kuabudu: Video 5 za Injili Zinazovuma Bongo
2 February 2021
[Photo Credit:Rose Muhando Instagram]
By Branice Nafula
Kwa miaka mingi sasa, nchi ya Tanzania imejulikana kuwatoa wasanii wenye vipaji hasa katika wimbo za kuabudu kwenye lugha ya Kiswahili.
Katika eneo Afrika Mashariki, Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo zinavuma kwenya tasnia hii.
Read Also: Rose Muhando Biography, Music Career, Awards, Family and Net Worth
Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano za kuabudu zilizofanya vizuri nchini Tanzania na eneo nzima la Afrika mashariki:
You are My Mountain - Rose Muhando
Katika wimbo wa ‘You’re my Mountain’, Rose Muhando anamsifu Mungu kwa kuwa chanzo chake cha nguvu. Kimsingi, wimbo huu unahimiza binadamu kumkimbilia Mungu kwani yeye tu ndiye anayeweza kutupigania katika shida zote. Kufikia sasa, wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki tatu kwenye mtandao wa YouTube.
Read Also: Rose Muhando Drops New Worship Song Dubbed ‘You are My Mountain’
Usinipite – Walter Chilambo
Katika muziki wa kuabudu Tanzania, Walter ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wameweza kubaki dhabiti, licha ya ushindani mkali kutoka kwa wenzao wanaoimba nyimbo za burudani.
Katika wimbo wake wa ‘Usinipite, Walter anamuomba Mungu asimpite wakati anapowatembelea wana wake.
Relax- Christina Shusho
‘Relax’ ni wimbo unaongazia kumuamini Mungu katika yote tuyafanyayo hapa duniani. Hivo Christina Shusho anasema ‘Relax’ (Tulia) kwani Mungu mwenyewe ana mipango yake na atatimiza. Kufikia sasa, wimbo huu una watazamaji zadi ya laki sita kwenye mtandao wa YouTube.
Mungu hapokei Rushwa - Goodluck Gozbert
Mungu Hapokei Rushwa ’hakika ni wimbo wa kukusaidia kujielewa kwa unadani zaidi. Licha ya kuwa wimbo wenye mdundo mzuri, 'Mungu Hapokei Rushwa' ni wimbo unaohusu uzuri wa Mungu na upendo wake usio na masharti.
Deni – Paul Clement ft Joel Lwaga
Kikawaida ahadi ni ‘Deni’ lakini kwa Mungu ni tofauti kwa kuwa kwake Mungu, ahadi sio deni sababu akiahidi lazima atimize.
Wimbo huu unatuhimiza kusubiri na kutegemea ahadi zake kwa kuwa ni za kweli na hatimaye hutimizwa.
Leave your comment