Stamina Amshirikisha Professor Jay na One Six Kwenye Wimbo Mpya ‘Baba’

[Photo Credit: Stamina Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii toka Tanzania wa fani ya Hip-hop Stamina, ameachia wimbo wake mpya kwa jina ‘Baba’.

‘Baba’ ni wimbo wake wa kwanza mwaka huu ambao amewashirikisha wasanii waliobobea Proffesor Jay na One six.

Katika wimbo wa ‘Baba’, Stamina anamkashifu babake kwa kumlea katika hali ya umasikini huku akisema kuwa amemdhalilisha yeye kama mwanawe.

“…Kwanza naomba ukae chini na uvute pumzi, na vitu vya kuonga ambavyo vitakuuzi, ivi unajua nimekuvumilia sana, angekua mtoto mwingine, tayara ungeshampa laana…” hii ni baadhi ya mistari yake Stamina.

Download Stamina Music for Free on Mdundo

Kwa kifupi, Stamina anaangazia namna watoto wanaeza walaumu wazazi kwa malezi mabaya.

Hivyo Stamina anamkashifu ‘Baba’ kwa kuwa mfano mbaya kwa wanae ambapo ameacha ulevi na starehe zikamharibia Mmaisha yake.

Kwa upande mwingine, Prof. Jay anamkumbusha huyu mwanawe anayemkashifu kuwa hana Asante. Anaelezea namna alivyohangaika hadi kuuza mali zake ili kumsomesha kijana huyo ili aje kuwasaidia wazazi wake.

Kama alivyoandika Stamina kwenye ukurasa wake wa Instagram “Vitu ambavyo wewe mtoto unamlaumu baba yako ndio vitu ambavyo mtoto wako atakulaumu wewe”.

Read Also: Rostam Biography, Music Career, Top Songs, Marriage, Net worth and Much More

Watatu hao walifanya kazi nzuri katika uandishi na hata kwa kuimba. Kanda ya wimbo huu pia ni ya kuvutia na kufikia sasa watu wameupokea wimbo huu kwa ukubwa sana. Katika mtandao wa YouTube “Baba” ina watazamaji Zaidi ya elfu hamsini na tano, dhihirisho kuwa ni wimbo umewagusa wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=_cim7dsia6Q

Leave your comment

Top stories

More News