Video Tano Moto Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Photo Credit:Nairobi News]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mziki wa bongo unaendelea kuimarika huku wasanii wakitumia mbinu mbali mbali kama kushirikisha wasanii kutoka fani zingine ile kueneza muziki wao.

Wiki iliyopita, wasanii kadhaa waliachia nyimbo mpya. Nakala hii inaangazia nyimbo tano zilizonawiri kwenye mtandao wa YouTube wiki hii:

Number One - Rayvanny na Zuchu

Katika ‘Number One’, Rayavanny na Zuchu wanathibitisha kuwa wao ni washirika wakamilifu kwani sauti zao hukamilishana kikamilifu. Kwa upande wake, Zuchu ameleta mguso wa Taarab na sauti yake. Huu ni ushirikiano wa kwanza kati ya wasanii hao wawili na kufikia sasa video hiyo ina watazamaji zaidi ya milioni mbili siku nne baada ya kuachiwa kwenye mtandao wa YouTube.

Read Also: Watch Rayvanny and Zuchu Get Cozy in New Number One Video

https://www.youtube.com/watch?v=8bQOuK95uYQ

Waah - Diamond akimshirisha Koffi Olomide

'Waah' ni wimbo unaoangazia mtu anayetetea mpenzi wa maisha yake. Diamond anaanza wimbo huo akielezea vizuri jinsi inavyohisi kupendwa, huku Koffi Olomide akitupia majigambo ya sauti yake. Wimbo huu umeletea jamii ya bara la Afrika mashariki hadhi kubwa sanaa baada ya kuvunja rekodi ya kuwa na watazamaji milioni 1 chini ya saa nane. Kufikia sasa wimbo huu unawatazamaji milioni moja Nukta tatu huku ikitarajiwa kuongezeka zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=HCuTwNgY3_M

Fall - Mbosso

Wimbo huu wa Mbosso unashikilia nambari tatu. Mbosso aliachia wimbo huu wiki iliyopita na kufikia sasa ni wimbo ambao unawatazamaji zaid ya millioni moja nukta tisa. Mbosso anaimbia mpenzi wake na kumjulisha hata mpenzi wake wa zamani kuwa yuko sawa sana.

Read Also: WCB Artists Takeover Bongo Music Scene with New Trending Hits

https://www.youtube.com/watch?v=Q8qWYve1gGs

Nibakishie - Nandy akimshirikisha Alikiba

Nandy alimshirikisha Alikiba ambaye kwa upande wake alidhihirisha ubabe wake katika mistari ya wimbo huu wa “Nibakishie” ni ushairi mzuri na mdundo wake pia ni ule wa RnB fani ambayo ni umahiri wa Nandy. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya milioni mbili nukta nne.

https://www.youtube.com/watch?v=UnxGYcoX7GI

Ushamba- Harmonize

Huu ndio wimbo wa mwisho wa Harmonize mwaka huu. Wimbo huu wa “Ushamba” unaendelea kupata uaarufu zaidi. Harmonize anawakashifu watu wennye tabia mbovu ya majisifu ambayo anaaita “Ushamba”. Wiki mbili baadae wimbo huu unawatazanji zaidi ya miliioni nne.

https://www.youtube.com/watch?v=sZ420sDOumE

Leave your comment