Zuchu Aweka Rekodi Mpya ya YouTube Nchini Tanzania

[Photo Credit: Zuchu Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii kutoka Wasafi almaarufu Zuchu anaendelea kuvunja rekodi za mziki wa bongo ambazo sio wengi wamefikia hata baada ya kuwa kwenye fani hii kwa muda mrefu.

Mwanamzuki huyo kutoka lebo ya Wasafi amefikisha wafuatiliaji (subscribers) zaidi ya 552,000 katika Mtandao wa YouTube. Rekodi hii imemfanya Zuchu kuwa Mwanamuziki wa kike mwenye subscribers wengi zaidi Afrika Mashariki huku Nandy akimfuta kwa ukaribu sana na wafuatiliaji 548,000.

Zuchu Drops New Song ‘Shangilia’

Zuchu kwa sasa ndani ya miezi saba katika mziki anaendelea kuachia mziki kila kukicha huku akiwa na tamasha kubwa kote nchini Tanzania.

Hii ni rekodi kubwa na ya kipekee kuifikia , hususan kwa mwanamuziki mwenye muda mfupi katika kiwanda cha muziki .

Mpaka sasa, Zuchu ana watazamaji zaidi ya milioni 64.8 katika chaneli yake ya YouTube, huku akiwa mwanamuziki wa kike anaeongoza kwa kutazamwa YouTube kwa miezi tano mfululizo nchini Tanzania.

Hata hivyo, Zuchu anavunja rekodi hizi kwa sababu ya bidii yake kubwa ambayo anatumia kukuza sanaa yake ya muziki. Hivi karibuni aliweza kuachia wimbo wake mpya “Nobody “ akimshirikisha msanii tajika kutoka Nigeria Joeboy.

Zuchu’s ‘Nobody’ Hit Featuring Joeboy Ranked among Top 10 Songs in Africa

Wimbo huu ulikua nyenzo ya Zuchu kupenyeza katika ukanda wa Afrika magharibi. Kwa wiki tatu sasa wimbo huo wa “Nobody” umetamba sana katika mtandao wa YouTube na kufikia sasa unawatazamji zaidi ya milioni mbili nukta saba.

https://www.youtube.com/channel/UCOn8zDM533kqzhIA8c3NFbQ/featured

Leave your comment