Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Video 5 Moto Zinazotamba Kwenye Mtandao wa YouTube Tanzania
27 October 2020

[Photo Credit:Zuchu Instagram]
By Branice Nafula
Wasanii wengi nchini Tanzania wanaendelea kutoa nyimbo mpya kila kukicha.
Wiki hii, video kadhaa zimevuma mitandaoni na kupata kutazamwa na watu wengi.
Baadhi ya video zilizofanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube wiki hii ni:
Nobody- Zuchu akimshirikisha Joeboy
‘Nobody’ ni wimbo wa kimapenzi ambapo Zuchu anamhakikishia Joeboy kuwa hamna anayempenda kama yeye, na kwa upande wake Joeboy anamhakikishia mapenzi ya dhati. Wiki moja baada ya kuachiliwa, wimbo huu unawatazamaji zaidi ya millioni mbili nukta tatu kwenye mtandao wa YouTube.
Litawachoma – Zuchu na Diamond
Wimbo huu umetazamwa zaidi ya mara milioni mbili kwenye YouTube chini ya wiki mbili. ‘Litawachoma’ ndio wimbo wa kwanza ambao Zuchu amemshirikisha mkuu wake Diamond Platnumz.
Download Diamond Music for Free on Mdundo
Do me - Nandy akimshirikisha Bilnass
‘Do me’ ni wimbo mzuri wa mapenzi kwa wanandoa wanaoelezea mapenzi yao kwa kila mmoja. Ukisikiliza toleo hili jipya, unahisi kuwa wasanii wote wanazungumza kutoka kwa mioyo yao kwani mapenzi yao ni ya kweli kisanii na katika maisha halisi. Kufikia sasa wimbo huu wa Bilnass na Nandy umepata watazamaji zaidi ya milioni moja.
Far away – Country wizzy akimshirikisha Harmonize
‘Far away’ ni wimbo wa mapenzi ambapo Country Boy anaangazia namna mpenzi wake anavyomfurahisha. Kufikia sasa wimbo huu wa Harmonize na Country Wizzy una watazamaji zaidi ya laki tano.
https://www.youtube.com/watch?v=dtpARfzLvIc&ab_channel=CountryWizzy
Haunisumbui - Diamond Platnumz
“Haunisumbui” ni wimbo wake Diamond akisimulia hadithi ya mpenzi wake wa kitambo ambaye amekuwa akimsumbua kwa muda baada ya mapenzi yao kuvunjika. Kulingana na Diamond, yule wa zamani hapaswi kuingilia maisha yake tena, kwani yote anayofanya kwa sasa hayamsumbui kamwe. Kwa sasa ni wimbo aina ya audio tu na umetazamwa zaidi ya mara milioni moj nukta saba.
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Joy Is Coming3:08
TUMWAMBIE MUNGU ASANTE0:49
Malaika2:49
NALOKINGA2:52
Stima - Buruklyn Boyz5:04
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Buwooma2:44
Alifata Hela3:53
Top stories
- NEW MANAGEMENT
01 April
- Love
01 April
- My biography
02 April
- STREAM NEXARITO SONGS ON SPOTIFY
02 April


Leave your comment