Nyimbo 5 Kali Zinazovuma Bongo Wiki Hii
23 September 2020
[Anwani ya Picha: The Citizen]
Mwandishi Omondi Otieno
Wasanii wengi nchi wanajitahidi kutoa nyimbo mpya na kuanda tamasha kila wikendi ili kurudisha pesa walizopoteza miezi kadhaa iliypopita baada ya janaga la corona kusitiza mikutano mikubwa.
Wki hii, video kadhaa zimevuma mitandaoni na kupata kutazamwa na watu wengi. Baadhi ya video zilizofanya vizuri ni:
Litawachoma – Zuchu na Diamond
Wimbo huu umetazamwa zaidi ya mara milioni mbili kwenye YouTube chini ya wiki mbili. ‘Litawachoma’ ndio wimbo wa kwanza ambayo Zuchu amemshirikisha mkuu wake Diamond Platnumz.
Wasted Energy – Alicia Keys na Diamond
Wimbo huu ni moja wapo ya nyimbo kutoka kwa albamu mpya ya Alicia Keys iitwayo ‘Alicia’. ‘Wasted Energy’ imetazamwa zaidi ya mara elfu mia tisa kwenye YouTube katika mda wa siku nne. Wimbo huu umezua utata nchi hasa kwa wafuasi wa Diamond ambao waligadhabishwa sana nayeye kupewa sekundi 26 pekee yake.
Ongeza – Diamond
Diamond aliachilia wimbo huu wikendi iliyopita. Kwa sasa, video yake bado haijaachiliwa. Kwenye mtandao wa YouTube, ‘Ongeza’ imetazamwa mara elfu mia nane kwa mda wa siku nne.
Sexy Mama – Lava Lava na RJ The DJ
Video hii ni mohja wapo kati ya nyimbo kutoka kwa albamu yake Romy Jons iitwayo ‘Changes’. Video hii iliachili wiki moja iliyopita na imetazwa zaidi ya mara milioni moja kwwenye YouTube.
Cheche – Zuchu na Diamond
Video ya wimbo hii imefutwa kwenye YouTube lakini toleo lisilokuwa na video bado lipo. Toleo hilo la ‘Cheche’ limetazamwa zaidi ya mara mia tisi kwenye YouTube.
Unapotazama nyimbo hizi zote, kile kinajitokeza ni kuwa kwa njia moja ama nyingine, zote zina uhusiano na lebo ya Wasafi chini ya uongozi wake Diamond Platnumz.
Leave your comment