Bifu la Meek Mill na Nicki Minaj laanza Upya, warushiana maneno

Source: Milard Ayo

Bifu la rapper Meek Mill na aliyekuwa mpenzi wake Nicki Minaj limerudi tena likiwa lamoto baada ya kurushiana maneno kwenye mtandao wa Twitter.

Sakata la kurushiana maneno lilianza baada ya LIKE ya Meek Mill kukutwa kwenye moja ya post ya mpenzi wa Nicki Minaj, Kenny Petty ambayo iliwekwa instagram na akaunti moja ya shabiki wa Nicki Minaj Post ambayo ilimfikia Nicki na kuanza kumchana Meek Mill akimtaka aendelee na maisha yake.

Nicki Minaj hakuishia hapo aliendelea kumrushia maneno Meek Mill kwa kumwambia ananyanyasa wanawake kwa kuwapiga, akitoa ushahidi kwamba alishawahi kumpiga Dada yake huku akijirekodi.

Tuhuma za kupiga wanawake hazikuwa nzuri kwa Meek Mill ambaye aliibuka na kujibu Tweets za Ex ambapo akajitetea kwa kusema sifa ya kuwapiga wanawake ndiyo kitu pekee Nicki Minaj anakitumia kutaka kuharibu karia yake.

Meek Mill akaenda mbali zaidi na kueleza jinsi Nick Minaj pia alivyowahi kushiriki kulipa fedha kutaka kesi ya kaka yake kuhusu kubaka kutaka ifutwe.

Source: Milard Ayo

Leave your comment