Lili Wayne kafunguka kuwa yeye anaasili ya Nigeria (+ video)

Source: Milard Ayo

Rapper kutoka Marekani Lil Wayne amesema yeye ana asili ya Nigeria kwa asilimia 53, jambo ambalo Mama yake mzazi hakuwahi kumwambia.

Lil Wayne amefunguka kwenye mahojiano na kipindi cha ‘Drink Champ’ ambapo watangazaji walimuuliza kwanini amewahi kuitaja Nigeria kwenye baadhi ya nyimbo zake za siku za nyuma?

Download FREE MP3 Music by Lil Wayne

Lil Wayne akajibu kwa kusema , “Shout out kwa Nigeria, Niliangalia asili yangu kwenye mtandao wa ancestry dot com na nikagundua nina asili ya Nigeria kwa 53%, Mimi na Mama yangu inabidi tuzungumze vizuri”. Lil wayne

Hata hivyo Lil Wayne aliongezea kwa kusema ataitembelea nchi ya Nigeria hivi karibuni. Bonyeza Play kumsikiliza akielezea.

Source: Milard Ayo

Subscribe to Top African Entertainment News

Leave your comment

Top stories