TANZANIA: The Mafik na Wakazi kwa mara ya kwanza kwenye Tamasha la ‘Sauti za Busara’

Source: Millard Ayo

Kila mwaka ifikapo February tamasha la muziki la Sauti za Busara hufanyika huko visiwani Zanzibar ambapo nchi mbali mbali hushiriki kushare burudani, fashion, tamaduni na hata maswala ya kijamii.

Download FREE MP3 - The Mafik

Kwa mwaka huu tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku nne ambapo ni kuanzia February 13 mpaka February 16 likiwa limebeba kauli mbiu ya ‘Paza sauti, kupinga vitendo vya kijinsia kwa wanawake”

Tamaha la Sauti za Busara la mwaka huu wa 2020 linatarajiwa kuepo na wasanii kutoka nchi tofauti tofauti watakao toa burudani yenye taste ya kila aina ya muziki utakao kuwa ukiimbwa Live na bendi.

Sehemu ya wasanii watakao burudisha ni pamoja na The Mafiki na msanii Wakazi kutoka Tanzania ambao wamezungumza jinsi watakavyo tumia fursa ya tamasha hili kutengeneza network na hata kolabo kutoka kwa wasanii wa mataifa tofauti tofauti.

“Nimefurahi ni opportunity nzuri kwangu Mimi, nitaweza kuonesha kile nilichonacho na nafasi ya kujifunza mengine kutoka kwa wasanii mbali mbali na naendelea kujipanga mpaka siku itakapo fika” – Wakazi

“Hii ni Mara yao ya kwanza toka kundi limeanza kama The Mafik, tuliomba kati ya waliotuma maombi wao wakachaguliwa baada ya vigezo vyao kuonekana vimekizi wao kuwepo Kwenye hili tamasha la sauti za busara wakachaguliwa, hili ni dili Lao kubwa sana toka nimeanza kuwa simama” – Meneja The Mafik

Source: Millard Ayo

Subscribe to Top African Entertainment News

Leave your comment