TANZANIA: Mtoto Wangu Akiiga Tabia Zangu Nitamsupport Tu – Gigy Money

Muimbaji Gigy Money amedai atajisikia furaha na amani kama mtoto wake wa kike aliyempa jina la Mayra kama atafuata nyayo zake katika maisha.Gigy ameiambia Enewz ya EATV kwamba, haiwezi ikatokea mtoto akawa na role model tofauti na mtu ambaye amemzaa.

“Kila mtoto yoyote ‘role model’ wake ni mama yake mzazi hata iwaje. Uwezi kusema mwanao atakuwa ‘role model’ wa mtu mwingine. Hivyo mwanangu atakuwa tu vyovyote atakavyotaka kuwa mimi nitampa ushirikiano. siwezi kumlaumu hata akitaka kuwa kama mimi ila ndio ntazidi kufurahi”, amesema Gigy.

Pamoja na hayo, Gigy ameendelea kwa kusema “siwezi kujutia kuzaa halafu kingine ni kwamba kujipanga utajipanga baada huko wala hupaswi kuwaza kuwa itakuaje nikifanya jambo fulani. Maisha ya siku hizi hayana hiyo kitu, Mungu yupo kila siku anatenda.”

Source: bongo5.com

Leave your comment